Mamlaka za mipango miji zatakiwa kutenga ardhi kwa ajili ya biashara, viwanda

April 4, 2019 12:49 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali imeandaa mwongozo wa tathmini ya mazingira kimkakati ambao utawezesha mpango wa uchumi na viwanda kufanyiwa tathmini ya mazingira kimkakati.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza imeziagiza mamlaka za upangaji miji zizingatie utengaji wa asilimia 10 ya kila eneo la mpango kabambe wa mji kwa ajili ya uwekezaji wa biashara na viwanda.

Majaliwa aliyekua akihutubia Bunge leo (Aprili 4, 2019) wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020 ambapo amesema katika mwaka 2018/2019, Serikali imeandaa mwongozo wa tathmini ya mazingira kimkakati ambao utawezesha mpango wa uchumi na viwanda kufanyiwa tathmini ya azingira kimkakati.

Amesema tathmini hiyo lazima iende sambamba na utengaji wa ardhi kwa ajili ya maeneo ya uwekezaji ili kuchochea ujenzi wa viwanda na uendelezaji wa viwanda.

“Katika maboresho ya kanuni yaliyofanyika, yanampa Waziri mwenye dhamana ya mazingira mamlaka ya kutoa vibali vya muda kwa ajili ya miradi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda na hivyo kuboresha taratibu za uwekezaji wa viwanda nchini,” amesema Mmajaliwa.

Amesemma ili kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia sekta ya viwanda, ekari 127,859 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya viwanda ambapo Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka za upangaji za Halmashauri za Wilaya za Kibaha na Kilosa, imetenga hekta 2,710 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vikubwa na vidogo.


Zinazohusiana: 


Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kuhuisha, kuboresha na kutekeleza sera, sheria, taratibu na mikakati ya maendeleo ya viwanda, biashara na masoko na kujikita katika uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini; kuimarisha na kusimamia mfumo wa biashara ya ndani na kutumia kikamilifu fursa za masoko.

“Serikali itaendelea kujenga uwezo wa taasisi za utafiti zinazohusika na maendeleo ya viwanda na kuhamasisha uanzishaji na maendeleo ya viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati,” amesema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, amesema sekta ya madini ina mchango  mkubwa katika kukuza uchumi, hivyo Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika kulinda rasilimali hizo kwa manufaa ya Watanzania kwa kutoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo na kuwakopesha zana za uchimbaji; kuwapatia utaalamu na matumizi ya teknolojia katika uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

Amesema katika mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kukuza soko la ndani la madini kwa kuvutia wawekezaji na kuhamasisha shughuli za uongezaji wa thamani madini nchini.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV