Mambo muhimu ya kuzingatia wakati unasafisha ‘pressure cooker’

June 13, 2025 4:37 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja kuepuka makosa ya kutumia sabuni au brashi zisizofaa ambazo huathiri utendaji wa pressure cooker

Pressure cooker ni kifaa muhimu katika maisha ya kisasa, hasa kwa wakazi wa mijini wanaohitaji kupika kwa haraka bila kupoteza virutubisho vya chakula. 

Ili kuhakikisha kifaa hiki kinaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kudumu kwa muda mrefu, usafi na uangalifu unahitajika ili kuepuka kujikusanya kwa mabaki ya chakula, harufu mbaya, na hata kuharibika.

Kwa mujibu wa chapisho la mwongozo wa mtumiaji wa jiko hilo lenye la WestPoint, zipo kanuni ambazo unapaswa kuzingatia wakati wa kusafisha.. 

Leo Jikopoint.co.tz tunakufahamisha hatua kwa hatua za njia ya kusafisha kifaa hiki ili kidumu kwa muda mrefu:

Anza kwa kuandaa kifaa

Kabla hujaanza kusafisha, hakikisha pressure cooker umeitoa kwenye plagi ya umeme na uiche kwa muda ili kuondoa joto. 

Hatua hii ni ya kiusalama na huepusha ajali zinazoweza kusababishwa na umeme au mvuke uliobaki ndani ya kifaa. 

Wakati huo huo, soma mwongozo wa mtumiaji wa kifaa chako kwani kila mtengenezaji anaweza kuwa na maelekezo mahsusi kuhusu usafi na utunzaji.

Suuza kwa maji ya uvuguvugu kabla ya kuosha

Baada ya kifaa kupoa, suuza sehemu ya ndani ya sufuria ya kupikia kwa kutumia maji ya uvuguvugu ili kulainisha mabaki ya chakula yaliyoganda na kuondoa harufu. 

Hii italifanya sufuria kuwa safi wakati wote na litadumu muda mrefu.

Tumia sabuni laini na sponji isiyochubua

Safisha sehemu ya ndani na nje ya sufuria kwa kutumia sabuni ya vyombo isiyo na asidi kali na sponji laini isiyokwaruza. Epuka kutumia vitu vigumu kama kisu, kijiko au brashi ngumu kutolea uchafu. Matumizi ya vitu hivi yanaharibu uso wa ndani wa sufuria na kuathiri uwezo wake wa kupika sawa sawa. 

Kwa madoa sugu, changanya kiasi kidogo cha ‘baking soda’ na maji ya sabuni kisha sugua taratibu mpaka uchafu wote utoke.

Safisha mpira ulipo kwenye mfuniko wa pressure cooker na valvu 

Vitu muhimu kama mpira wa kufunga (gasket) na valvu ya kutoa mvuke vinapaswa kutolewa kwa uangalifu na kusafishwa kando kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye sabuni.

Kwa sehemu ambazo ni ngumu kufikiwa, unaweza kutumia brashi laini ili kuhakikisha kila sehemu imesafishwa vizuri. 

Mpira ukiachwa na mabaki ya chakula unaweza kupoteza uimara wake na kuvuja wakati wa kupika.

Kausha vizuri kabla ya kuhifadhi

Baada ya kila sehemu kusafishwa kikamilifu, hakikisha unakausha kwa kitambaa kisafi. 

Kwa upande wa jiko, iwapo kutakuwa na uchavu tumia kitambaa kufuta na hakikisha unaepuka kutumia maji wakati wa kusafisha ili kuzuia kutu ambazo huenda zikaharibu jiko.

Usihifadhi pressure cooker ikiwa na unyevu kwani hali hiyo huweza kusababisha kutu hasa sehemu za ndani.Baada ya hapo hifadhi kifaa chako mahali pakavu na salama. 

Kwa kufuata hatua hizi za msingi utadumisha ubora wa kifaa chako, kuepuka gharama zisizotarajiwa za matengenezo na kuhakikisha chakula chako kinapikwa katika mazingira safi na salama. Kama bado hujamiliki pressure cooker, jikopoint.co.tz inaambaza chapa ya WestPoint kwa bei nafuu. Kwa maelezo, wasiliana nasi kupitia namba 0677088088.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
12 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV