Majaliwa atoa onyo matumizi yasiyo sahihi ya Tehama kwa vijana

October 12, 2021 1:40 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Maadhimisho haya yanalenga kuwakumbusha na kuiwezesha jamii na Taifa kwa ujumla kutambua mchango mkubwa wa vijana katika maendeleo ya nchi na kuwapa fursa nyingi vijana kumuenzi na kumkumbuka Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Picha| Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Awataka wajiepushe na utapeli, wizi wa mtandaoni.
  • Pia wajiepushe na uchachezi na kutunza amani ya nchi.
  • Vijana watakiwa kutumia Tehama kujikwamua kimaisha.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi hususani vijana wajiepushe na matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo wizi, utapeli wa fedha n auchochezi unaofanywa kwa njia ya mtandao.

Pia amewaasa vijana nchini wajiepushe na kujiunga na makundi yasiyofaa, kujiingiza kwenye majukwaa ya uchochezi kwani vitendo hivyo vinavuruga amani, utulivu na mshikamano wa Taifa.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Oktoba 12, 2021 alipozindua maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa katika viwanja vya Mazaina wilayani Chato mkoani Geita.

“Kutokana na umuhimu huo Serikali imesisitiza matumizi sahihi ya Tehama kwenu vijana kwani ninyi ndiyo watumiaji wakubwa na wahanga wakubwa wa Tehama,” amesema Majaliwa.

Badala yake amewataka kutumia Tehama kama nyenzo ya kujiajiri na kufanya shughuli zitakazowasaidia kuboresha maisha yao kwa sababu ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.

“Vijana wengi wamefanikiwa kutokana na matumizi sahihi ya Tehama hususan kwa kufanya biashara kwa njia ya mtandao. Vijana wameweza kuanzisha na kuendesha vituo vya huduma za intaneti na pia kuanzisha wakala wa huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu,” amesema Majaliwa.

Aidha, amewataka vijana watumie fursa zilizopo nchini katika kujiletea maendeleo na kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira inayoikabili dunia kwa sasa. 

“Tanzania tunayo ardhi ya kutosha na yenye rutuba, tuna bahari, tuna maziwa na mito mikubwa, tunayo madini pia tunayo fursa ya uhusiano mwema wa kidiplomasia na nchi zote duniani,” amesema Majaliwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tixon Nzunda amesema wiki ya vijana imeanzishwa kwa lengo la kuwakutanisha na kuwapa nafasi vijana na wadau wa shughuli za maendeleo yao kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali yanayowahusu kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Amesema maadhimisho hayo ambayo yalianza Oktoba 8, 2021 na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14 yamehudhuriwa na vijana zaidi 1,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao pamoja na mambo mengine wamepata mafunzo ya aina mbalimbali yakiwemo na ya matumizi bora ya Tehama.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV