Majaliwa afuta mnada wa nafaka mtandaoni

January 10, 2020 4:11 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ule ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Januari 7, 2020.
  • Mnada huo ambao unahusisha mahindi na ngano ulifanyika baada ya wahusika kushindwa kutimiza masharti ya kiforodha.
  • Majaliwa asema taratibu za kutangazwa zabuni hazikufuatwa. 

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefuta mnada wa nafaka ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Januari 7, 2020 na kuuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kutangaza upya zabuni baada ya kutoridhishwa na taratibu zilifanyika awali.

Mnada huo ambao unahusisha mahindi tani 5,000 na ngano tani 460.12 unafanyika baada ya wahusika kushindwa kutimiza masharti ya kiforodha, hivyo Serikali imeamua kuuza ili kufidia gharama zake. Nafaka hizo ziliingia nchini Machi 2017.

Majaliwa amesitisha mnada huo jana (Januari  9, 2020) wakati akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA,  Ben Asubisye katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu,  ameagiza kutangazwa upya kwa mnada mwingine wa kuuza mahindi hayo sambamba na ngano na wahakikishe masuala yote kuhusu mnada huo yanakamilika ndani ya siku tatu kuanzia jana  Januari 9, 2020.

“Mahindi yameuzwa kwa bei ya Sh340 kwa kilo moja ambayo ni chini na bei ya soko kwa sababu bei ya mahindi sokoni kwa sasa ni Sh800 (kwa kilo). Zabuni imetangazwa kwa muda mfupi watu wameshindwa kushiriki. Ilifunguliwa saa 8 mchana na imefungwa saa 5 usiku,” amesema Majaliwa katika taarifa hiyo.


Zinazohusiana:


Aidha, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa TRA uhakikishe mnada unaofuata unakuwa wa wazi, huru pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa wananchi wote kushiriki ili kuondoa malalamiko. 

“Kwa kuwa mnada unafanyika kwa njia ya mtandao, hakikisheni matumizi ya mtandao yanakuwa rafiki kwa wananchi wote watakaovutiwa kuwasilisha zabuni zao,” amesisitiza Majaliwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa TRA ishirikiane na mamlaka nyingine za Serikali kuhakikisha wanunuzi wa nafaka hizo hawaziingizi sokoni kwa ajili ya matumizi ya binadamu. 

Nafaka hizo zimepimwa na kuthibitika kuwa zinafaa kwa matumizi ya wanyama

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.