Magufuli, TMA wazungumzia mafuriko Lindi

February 13, 2020 3:58 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema wananchi wachukue tahadhari kwa sababu mvua bado zipo.
  • Yasema waepuke mazoea ya misimu ya mvua iliyozoeleka miaka ya nyuma ili kujikinga na athari zinazoweza kutokea.
  • Rais Magufuli awataka wanaoishi mabondeni wahama kuepuka mafuriko.  

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi kuepuka tabia ya mazoea ya misimu ya mvua iliyozoeleka miaka ya nyuma na kutakiwa kuchukua tahadhari ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo ongezeko la joto na mafuriko.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi aliyekuwa akizungumza leo (Februari 12, 2020) katika warsha ya wanahabari amesema mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na wakati mwingine kwenda kinyume na matarajio ya jamii.

“Naendelea kusisitiza jamii kuwa bega kwa bega na TMA na kuepuka tabia ya kuwa na  mazoea ya misimu ya hali ya hewa iliyozoeleka huko miaka ya nyuma, hasa ikizingatiwa kwamba mabadiliko ya tabia nchi yana athari katika mifumo ya hali ya hewa na hivyo kubadilika kwa misimu,” amesema Dk Kijazi.

TMA inatambua madhara yaliyotokana na hali mbaya ya hewa katika maeneo mbalimbali hapa nchini hivi karibuni ikiwemo mafuriko yaliyozikumba kaya mbali mbali katika mkoa wa Lindi na maeneo mengine nchini.


Zinazohusiana.


“Mamlaka inatoa pole kwa wote walioathirika na mafuriko hayo na kuwaomba watanzania wote wawe wanafuatilia taarifa za hali ya hewa pamoja na tahadhari zinazotolewa na TMA ili kupunguza athari zinazoweza kutokea,” amesema Dk Kijazi.

Taarifa hizo zinazotolewa kila siku zikitumika kwa usahihi na wananchi na taasisi zinazosimamia sekta mbalimbali ni pamoja na vipindi vifupi vya mvua kubwa zinazoweza kuharibu miundombinu na kusitisha huduma za kiuchumi na kijamii.

Naye, Rais John Magufuli amewataka wananchi wote wanaoishi mabondeni kuondoka ili kuepuka uharibifu kwasababu mvua bado zinaendelea kunyesha.

“Niwaombe wote wanaojenga kwenye mabonde Tanzania nzima waache waondoke wenyewe, wayaachie maji yapite na mabonde tuyatumie kwa ajili ya kulisha mifugo yetu na kulima lakini si kwa ajili ya makazi,” alisema Rais Magufuli jana (Februari 11,2020) katika uzinduzi wa jengo la Halmashauri ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Aidha, alisema Serikali haitatoa msaada kwa watakaokaidi kwa sababu mabondeni siyo sehemu ya kuishi.

/
No matches found for this filter
10 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
10 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
10 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Nukta TV

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV