Maboresho sekta ya sheria yaokoa Sh9.01 bilioni za kuwalipa mawakili

June 18, 2019 12:58 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Hata hivyo, amesema Serikali itaendelea kutumia mawakili binafsi kwa kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale itakapothibitika kuwa ni lazima kufanya hivyo. Picha|Mtandao.


  • Fedha hizo zimeokolewa mwaka 2018/2019 baada ya kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. 
  • Awali Serikali ilikuwa inatumia kampuni binafsi za uwakili kuendesha mashauri. 
  • Imesema katika baadhi ya mashauri itaendelea kuwatumia mawakili binafsi. 

Dar es Salaam. Kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika sekta ya sheria nchini, Serikali imeeleza kuwa imefanikiwa kuokoa takriban Sh9.01 bilioni ambazo zingetumika kulipa makampuni binafsi ya uwakili kuendesha mashauri ya taasisi za Serikali. 

Baadhi ya maboresho hayo ni kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia, kuendesha na kuratibu mashauri yote ya madai kwa niaba ya Serikali.

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga ametoa maelezo hayo Bungeni leo (Juni 18, 2019) wakati akijibu swali la Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ambae alitaka kujua kiasi cha fedha ambacho serikali imeokoa tangu maboresho kwenye sekta hiyo yaanze kutekelezwa.

Dk Mahiga amesema katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 pekee Serikali imeweza kuokoa takriban Sh9.01 bilioni ambazo kama siyo maboresho kwenye sekta hiyo zingetumika kulipa makampuni binafsi ya uwakili. 


Soma zaidi:


Hata hivyo, amesema Serikali itaendelea kutumia mawakili binafsi kwa kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale itakapothibitika kuwa ni lazima kufanya hivyo. 

Ametoa mfano wa vigezo vinavyotumika kutumia mawakili binafsi ni pamoja na shauri kufunguliwa katika mahakama ambazo siyo za kimataifa na sheria za nchi husika haziruhusu uwakilishi wa Mwanasheria kutoka nje ya nchi hiyo. 

Katika kuhakikisha maslahi ya Taifa yanalindwa, Waziri huyo ameliambia Bunge kuwa uendeshaji wa mashauri hayo utaendelea kuishirikisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye kila hatua ya mwenendo wake tofauti na hapo awali. 

Kuhusu baadhi ya mashirika ya umma kuendelea kutumia mawakili binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amesema mashirika hayo ni yale ambayo mashauri yake yalianza kabla ya maboresho hayo hayajaanza kutekelezwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV