Kompyuta bora zinazowafaa wanafunzi vyuo vikuu Tanzania

October 9, 2021 10:17 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Zina uwezo mzuri wa betri na skrini ya kutosha kusomea.
  • Gharama zake siyo haba lakini sifa zake zinaeleweka.

Dar es Salaam. Ni miezi michache kuelekea mageti ya vyuo vikuu nchini Tanzania kufunguliwa ili kuruhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza waanze masomo.

Mbali na kalamu, daftari na kikokotoo, zana nyingine muhimu chuoni ni kompyuta binafsi (laptop)ambayo itakusaidia katika kukamilisha majukumu yako ya kila siku ikiwemo kazi, kuandaa mawasilisho na hata kujisomea.

Kutokana na mahitaji ya wanafunzi, hizi ni baadhi ya kompyuta bora kwa matumizi ya shule na vyuo:

Dell XPS 13 

Kwa wanafunzi wa chuo, wanahitaji kompyuta ambayo siyo nzito. Inayoweza kubebeka kwenye begi  ikiambatana na madaftari.

Dell XPS 13 ambayo gharama yake ni Sh3.1 milioni inafikia vigezo hivyo.

Mbali na wepesi, kompyuta hii ya uzao (generation) wa 11 ina uhifadhi wa jigabaiti nane hadi 32 (GB8-GB32) ambazo kwa mwanafunzi, zinamtosha lakini kwa wanaopenda kuangalizia filamu huenda isiwe mahususi.

Dell ni nyepesi na utendaji kazi wake ni mzuri. Picha| Dell.

HP Envy x360

Kwa mwanafunzi mwenye matumizi ya muda mrefu ya kompyuta, hii inamfaa kwani inatajwa kuwa kati ya kompyuta zinazokaa na chaji kwa muda mrefu zaidi. 

Kwa mujibu wa tovuti ya HP, envy inapatikana kwa Sh1.4 milioni huku ikiwa na uwezo wa kukunjika kwa nyuzi 360.

Surface Laptop 4

Kwa anayetafuta kompyuta rahisi kutumia na isiyo na mambo mengi, Surface Laptop 4 yenye gharama ya Sh2.3 milioni inaweza kumfaa.

Kuanzia skrini kubwa na uhifadhi wa hadi GB512, kompyuta hii inaweza kumfaa mwanafunzi kwa kazi hata nje ya chuo.

HP Envy inakunjika kwa nyuzi 360. Picha| The Verge.

HP Spectre x360

Hii nayo gharama yake ni Sh2.6 milioni lakini utapata thamani ya pesa yako.

Spectre x360 ni ya uzao wa 11Intel ikiwa na prosesa ya Core™ i5. Inaambatana na uhifadhi wa kuanzia GB8 hadi GB256.

Ina skrini ya kupangusa kama zilivyo simu janja na ukubwa wake ni inchi 13.5.

Spectre pia inatajwa na wadau wa teknolojia kutoka The Verge kuwa na muonekano mzuri huku uwezo wa betri wake pia ukiipa thamani pesa yako.

Acer Swift 3

Ni kompyuta yenye thamani ya Sh1.7 milioni inayotumia mfumo endeshi kuanzia Window 10. Mbali na kiandikio (keyboard) kinachowaka, kompyuta hii inamfaa mwanafunzi kwa kuwa na uhifadhi mkubwa wa RAM ya GB8 na uhifadhi wa kawaida wa GB256.

Ina Sehemu kwa ajili ya kuskani alama za vidole na ina ukubwa wa inchi 14.

Unaweza kununua na kurudisha kama haifai ndani ya siku 30. Ni nyembamba na imetengenezwa kwa malighafi ya chuma huku betri lake likiwa na uhakika wa kutumika hadi saa 11 kulingana na matumizi.

Kama kuhusu mikopo tumekuhabarisha, na sasa kompyuta. Unataka nini tena? Endela kufuatilia www.nukta.co.tz.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW