Jinsi ya kurejesha mafaili yaliyofutika kwenye Windows 10 na 11

December 20, 2024 10:27 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa kutumia programu zinazopatikana bure na nyingine za kulipiwa.
  • Programu hizo ni pamoja na Recuva na Microsoft’s Windows file recovery.

Dar es Salaam. Huenda umewahi kufuta faili muhimu kwenye kompyuta, flashi au kadi kadi ya kuhifadhia data na ukahitaji kuzirejesha bila mafanikio.

Ikiwa umekutana na tatizo hili usijali, zipo njia za kurudisha faili  au nyaraka uliyoifuta kimakosa hata kwenye ‘recycle bin’ ambayo ni tegemeo la mwisho la kuhifadhi taarifa katika kompyuta.

Kwa mujibu wa tovuti maarufu ya habari za teknolojia ya ZDNET mafaili yaliyofutika yanaweza kurudishwa kwa njia ya programu tumizi zinazopatikana kwenye ‘Microsoft store’ na nyingine za kupakuliwa kutoka tovuti za mtandaoni.

Mbinu ya kwanza iliyozoeleka kwa wengi ni kuanza kufungua ‘recycle bin’, programu ambayo kwa kawaida faili linapofutwa huingia kabla ya kufutika kabisa kutoka kwenye kompyuta. 

Kisha tafuta faili lako kwa kutumia kisanduku cha utafutaji au kwa kupanga mafaili kwa jina na tarehe ili kupata lililopotea alafu bonyeza kulia kwenye faili na uchague kipendele cha ‘Restore’ kitakachokuwezesha kurudisha faili mahali lilipokuwa awali.

Ikiwa faili lako halipo kwenye ‘recycle bin’, usijali kwa sababu unapofuta faili kwenye kompyuta yako, haimaanishi kwamba limefutika kabisa, tuchukulie faili kama mchoro kwenye karatasi ya daftari, unapoufuta unakuwa umeondoa sehemu ya maudhui ya daftari hilo lakini kurasa unayoweza kuchora tena bado ipo. 

Hivyo ndivyo mfumo wa kompyuta unavyotoa nafasi ya wazi kwaajili ya kurudisha tena faili jipya kwenye nafasi ya faili hilo lililofutwa.

Microsoft’s Windows file recovery

Njia nyingine ni kutumia programu tumishi inayopatikana bure ‘Microsoft store’ kwa ajili ya kurudisha mafaili yaliyofutika kabisa.

Baada ya kuipakua na kuisakinisha (install) bofya ikoni ya programu hiyo ili ifunguke, kisha itakuletea maandishi yanayoonyesha jinsi ya kutumia programu hiyo hatua kwa hatua.

Programu hii hufanya kazi kupitia maandishi (command prompt), hivyo itabidi ujaze mahali ambapo faili lilifutwa (mfano, C:\Users\Documents) alafu uweke sehemu unayotaka faili zilizorudishwa zihifadhiwe na umalizie njia ya kurejesha (regular) kwa urejeshaji rahisi au “extensive” kwa uchambuzi wa kina.

Screenshot zikionesha mwenekano na mfano mwa matumizi wa programu ya Microsoft’s Window file recovery. Picha |Davis Matambo

Kisha programu itajaribu kutafuta na kurejesha faili zako kutoka kwenye sehemu zilizofutwa. Kama itakusumbua kutumia, angia ukurasa wa msaada wa Microsoft usome jinsi ya kutumia programu hiyo.

Tumia programu ya ‘Recuva’

‘Recuva’ ni programu mahususi ya kurejesha faili zilizofutwa inayopatikana mtandaoni kupitia tovuti yake. Kwanza, pakua na usakinishe programu hiyo kwenye kompyuta yako. 

Ukishaifungua, programu itakuongoza hatua kwa hatua, itaanza kukuuliza aina ya faili unazotaka kurejesha, kama ni picha, nyaraka, au video na mahali ilipofutwa kama ni kwenye diski kuu au USB.

Baada ya kuchagua, bonyeza ‘Scan’ ili programu ianze kutafuta faili hizo na Ikikamilisha, utaona orodha ya faili zilizofutwa ambapo utataikwa kuhagua faili unazotaka kurejesha na kubonyeza kitufe cha “Recover” kisha utabonyeza sehemu ya kuhifadhi faili hizo mpya.

Mwonekano wa skrini ya matokeo ya urejeshaji wa faili zilizofutwa au kupotea ikionyesha maelezo ya jina, njia, ukubwa, na hali ya urejeshaji. Picha |Recuva

‘Glarysoft file recovery free’

Hii ni programu nyingine ya bure inayoweza kurejesha faili zilizofutwa kutoka kwenye ‘recycle bin’ au kwa sababu nyingine kama kufuta kwa bahati mbaya, hitilafu za mfumo, mashambulizi ya virusi, kufutwa makusudi kwa data kwenye diski, na hitilafu za programu.

Anza kwa kupakua programu kwenye tovuti yake mtandaoni na uisakinishe kwenye kompyuta yako. Baada ya hapo fungua programu na chagua sehemu ya diski unayotaka kutafuta faili zilizofutwa. 

Programu itachanganua diski hiyo na kuonyesha orodha ya faili ambazo zinaweza kurejeshwa. Kisha, chagua faili unayotaka na ubofye kitufe cha kurejesha ili kuhifadhi faili hiyo mahali pengine kwenye kompyuta yako unapoona ni salama.

Skrini ikionyesha mchakato wa kutambua na kurejesha faili zilizopotea au kufutwa, ikiwa na maelezo kama njia ya faili, aina ya faili, ukubwa na tarehe. Picha |Glarysoft File Recovery

WinfrGUI

Kwenye orodha yetu programu ya mwisho yenye urahisi kwa kurejesha mafaili yaliyofutwa ni hii ambayo utaratibu wake hufanya kazi kama programu nyingine ambazo ni lazima kuipakua na sakinisha kwenye kompyuta yako.

Baada ya hapo ifungue na chagua sehemu (kama diski au kifaa cha kuhifadhi) unayotaka kutafuta kwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa ‘start recovery’. 

Skrini ikionyesha aina za faili na folda zinazoweza kurejeshwa sambamba na hali ya utafutaji ‘Quick Scan’ kwa utafutaji wa haraka na ‘Deep Scan’ kwa utafutaji wa kina. Picha |WinfrGUI

Baada ya utafutaji kukamilika, utaona orodha ya mafaili yaliyopatikana. Chagua faili unalotaka na bonyeza kitufe cha kurejesha ili kuhifadhi tena faili hilo mahali pengine salama.

Enable Notifications OK No thanks