Jinsi ya kukabiliana na tatizo la kuharibika kwa mimba

November 23, 2020 12:58 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Tatizo hilo husababishwa na mambo mengi ikiwemo uzito uliopitilizwa ama mjamzito kupigwa tumboni.
  • Pia, uvimbe kwenye kizazi huweza kuwa sababu ya baadhi ya wanawake kukubana na changamoto hiyo.
  • Baada ya kukumbana na tatizo hilo, mtu anashauriwa kutumia dawa kwa kuzingatia maelezo aliyopewa na mtoa huduma za afya.

Dar es Salaam. Kupata watoto baada ya kuingia kwenye ndoa ni moja ya malengo ya wanandoa wengi wengi. 

Lakini suala la kupata mtoto huusisha mchakato mrefu ambao unahitaji umakini hasa kwa mama mjamzito ili kuepusha mimba kuharibika na hatimaye kutoka kabla ya wakati. 

Kuharibika kwa ujauzito husababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo matatizo katika maumbile ya mfuko wa uzazi. 

Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Tanzmend, mimba huharibika kutokana na kutokuwepo kwa uwiano wa vichocheo (hormonal inbalance) hasa upungufu wa kichocheo aina ya “progesterone” ambacho ni muhimu sana katika ukuaji wa mimba.

Sababu zingine ni pamoja na uvimbe kwenye kizazi, kulegea kwa shingo ya kizazi, mjamzito kuwa na kinga ya mwili dhaifu, kufanya kazi ngumu na kwa muda mrefu, kupigwa kwa mjamzito kwenye tumbo, utapiamlo na uzito uliopitiliza.

Dalili za kuharibika kwa mimba

Tanzmed imeainisha kuwa “kutokwa damu kwenye sehemu za siri za mwanamke ambapo huanza kama matone na baadaye kuongezeka kuwa nyingi, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, homa na ulegevu pamoja na maumivu ya kiuno.”

Ufanye nini endapo hali hiyo imekukuta? Tazama video hii kujifunza zaidi:

Enable Notifications OK No thanks