Jinsi ya kuandaa uji wa tende na maziwa

March 11, 2025 4:31 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Uji huu ni unaweza kuwafaa waliopo katika mfungo wa Kwaresma au ramadhan.
  • Una virutubisho vyote muhimu vinavyoweza kukufanya uimarike upya baada ya swaumu ya kutwa nzima.

Baada ya saa kadhaa za kufunga, si kila kinywaji kinaweza kukuburudisha na kupa mwili wako virutubisho vinavyouhitaji ili kujiandaa kwa ajili ya kufunga kwa siku nyingine.

Kubali au ukatae ila vinywaji ndiyo vinaweza kurudisha nguvu iliyopotea mwilini kwa haraka ikiliandaa tumbo kwa ajili ya kupokea chakula kizito hususani kikiwa cvha moto.

Miongoni mwa vinywaji hivyo ni uji wa ulezi wenye  tende na maziwa uliosheheni virutubisho vingi ambavyo vitauimarisha mwili wako vikiliandaa tumbo kupokea futari nzito iliyoandaliwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya masuala ya afya ya Healthline, ulezi husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kweye damu, kupunguza lehemu (cholesterol) pamoja na shinikizo la damu.

Pia, kinywaji hicho kikichanganywa na maziwa kinaweza kuimarisha afya ya mama mjamzito pamoja na mtoto anayeanza kula kutokana na wingi wa madini chuma na kalsiamu.

Ili kupata faida hizo za kiafya, jikopoint imekuandalia hatua za maaandalizi ya uji huo unaoweza kuutumia wakati wa mfungo huu wa Ramadhani kwa waislamu na mfungo wa kwaresma kwa wakristo.

Hatua za kuandaa uji wa tende na maziwa

Anza kwa kuondoa mbegu katika tende kisha ziosha uloweke kwenye maji kwa dakika 30 ili zilainike. Baada ya hapo, saga hadi upate uji mzito wenye ladha tamu asilia.

Htua inayofuata ni kuandaa uji ambapo tutatumia maziwa badala ya maji, ambapo utabandika maziwa jikoni ikifuatiwa na uji wa tende na kabla hayajachemka changanya unga wa ulezi na maji katika kikombe au bakuli pembeni na kisha umimine jikoni.

Koroga bila kuachia kwa muda wa dakika 10 kwa moto mdogo mdogo hadi uji uoneshe dalili za kuanza kuchemka na uongeze robo kijiko cha hiriki kama unapendelea.

Kama hupendelei maziwa ya ng’ombe unaweza kuchemsha uji wako kwa kutumia maji ya kawaida au ukatumia aina nyingine ya maziwa ikiwemo ya almondi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
12 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV