Jinsi ya kuandaa ‘sandwich’ ya mboga mboga nyumbani

October 23, 2024 2:13 pm · Mlelwa Kiwale
Share
Tweet
Copy Link
  • Kitafunwa hiki unaweza kuwatengenezea watoto na hata kukibeba kwenda nacho ofisini.

Teknolojia imefanya mkate uandaliwe kwa namna tofauti kulingana na mazingira au mahitaji ya mlaji.

Siku hizi kuna mikate ya kukaushwa au ‘toasted bread’ ambayo hupitishwa katika kifaa maalum na kuifanya mikate kuwa na rangi nzuri ya kahawia pia kuna mkate aina ya ‘Sandwich’ ambayo pia huandaliwa kwa aina yake kwa kutumia vifaa maalum.

Licha ya uwepo wa vifaa hivyo unaweza kuandaa sandwich nyumbani kwa urahisi na kuepuka gharama kununua kitafunwa hicho mara mara katika migahawa au hotelini.

Unaweza pia kutengeneza kitafunwa hicho kwa kuwafurahisha uwapendao iwe ni watoto au wageni watakaokutembelea.

Ili kutengeneza kitafunwa hiki nyumbani utahitaji mkate, kitunguu maji, nyanya, tango,parachichi, pilipili manga, siagi, jibini, bila kusahau kikaangio na jiko la kupikia.

Baadhi ya mahitaji ya kuandaa sandwich, unaweza kuongeza au kupunguza kadri utakavyo.Picha Eat Well.

Maandalizi

Hatua ya kwanza andaa viungo kwa kuviosha na kuvikatakata kwa umbo la duara kisha kuvihifadhi pembeni.

Baada ya hapo chukua vipande vya mkate (unaweza kutumia mkate wa aina yoyote uwe mweupe au wa kahawia) vipake siagi  kisha uwashe jiko na kubandika kikaango tayari kwa kuanza maandalizi ya sandwich.

Kikaango kikipata moto weka siagi kiasi kisha weka kipande kimoja cha mkate.

Muonekano wa sandwich baada ya maandalizi kukamilika.Picha|Swatchi Recipes.

Anza kupanga viungo kwa kuanzia kitunguu maji, nyanya, tango, parachichi, jibini, pilipili manga na kumalizia kipande cha pili cha mkate ambacho umekipakazia siagi pia.

Hakikisha moto uwe kiasi ili usiunguze mkate huo huku ukiwa unageuza kila upande hadi vibadilike na kuwa rangi ya kahawia.

Ukimaliza epua sandwich  ikate kati iwe katika shepu ya pembe tatu na hapo itakuwa ipo tayari kwa kuliwa.

Kitafunwa hiki unaweza kukiandaa muda wowote iwe ofisini, mashuleni, kuwaandalia watoto, familia pamoja na kusukumia kwa kinywaji chochote ukipendacho.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV