Je unajua asilia ya mwito wa simu ya Nokia ?
Ukimuliza mtumiaji yoyote wa simu atakwambia pasipo shaka mwito wa simu ya Nokia Nokia tune maarufu kama Gran Valsk ni moja ya mito katika simu kwenye miaka ya 1990s iliyopata umaarufu mkubwa sana.

Mwitikio wa Nokia(Nokia tune)
Mwaka 1993 Anssi Vanjoki, Makamu wa Rais wa kamapuni ya Nokia walitambulisha tune hiyo ya Gran Valsk kwa Kivinen wakati huo akiwa mkuu wa mawsiliano ndani ya kampuni hiyo na kwa pamoja waliuchagua wimbo kuwa mwitikio wa simu Nokia .
Mwitikio huo “ Gran Vals” ulitungwa na kupangiliwa na solo gitaa na mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo wa kihispanialo Francisco Tárrega, ikiwa ni miaka 91 toka ulipotungwa mwaka 1902 na kuanza kutumiwa na Nokia.

Francisco Tàrrega (before 1900
Mwanzoni miaka ya 1990s kwa mara ya kwanza wimbo au mwitikio wa Nokia ulisikika kwa sekunde 3.Na ukazaa kuwekwa kwenye simu kwa mara ya kwanza kwenye Nokia 2110 ambayo ilitolewa mwaka 1994 chini ya jina la ringitone Type 7 ,kuonyesha kuwa kuwa ilikuwa ni mwito wa simu wakawaida.
Nokia 2110
Asili ya mwitiko huo ulikuwa unatofautiana kwenye listi ya mwito wa simu wakati mwingine ikitajwa kama Type 13 kwenye baadhi ya simu na simu nyingine kama Type 5.
Mwaka 1997 baada ya simu aina ya NOKIA 6110 6110 kutambulishwa sokoni ,kila mwito wa simu ulipewa jina maalumu na hapa ndio jina maarufu kwa sasa mwito wa Nokia (Nokia tune) ulipo anza,ingawa kabla ulikuwa ukiitwa Grande valse.Ni mwaka huo 1999 Grande Valse ulibadilishwa jina na kuwa Nokia Tune na muda huo huo ukawa ndio mwito na alama kwenye simu za Nokia.
NOKIA 6110
Latest