Innoss’B awapiga kikumbo wasanii wa Bongo Fleva Tanzania
- Ameshikilia nafasi ya kwanza kama msanii aliyetazamwa zaidi nchini Tanzania katika mtandao wa YouTube akitokea nafasi ya 26 aliyoshika wiki iliyopita.
- Amemshusha Harmonize kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tatu.
- Hakuna msanii wa kike wa Tanzania aliyeingia tano bora huku Nandy na Nora wawakilisha wasanii wa kike kwenye orodha ya 20 bora.
Dar es Salaam. Mchuano baina ya wasanii wa muziki Tanzania ukiwemo wa Bongo Fleva kwenye mtandao wa YouTube umekuwa wenye ushindani hasa baada ya wasanii wengi kutoa nyimbo zao siku za hivi karibuni.
Mchuano huo ni kuvutia watazamaji wengi na kung’ang’ania kileleni katika chati ya YouTube ya wanamuziki, nyimbo zinazofanya vizuri kwenye mtandao huo.
Hata hivyo, huenda mchuano kati yao ukazidi kuwa wenye ushindani baada ya nafasi ya kwanza ya wasanii wanaofuatiliwa nchini kushikiliwa na msanii toka nje ya nchi.
Ifuatayo ni orodha ya wasanii watano wanaofuatiliwa zaidi nchini Tanzania katika mtandao wa Youtube kufikia leo (Septemba 17, 2019).
5. Ali Kiba
Baada ya kupanda kutoka nafasi ya 16 wiki iliyopita, Alikiba amepata ya watazamaji milioni 3.43 kwa wiki hii waliofuatilia nyimbo zake. Watazamaji hao wametafuta zaidi wimbo wa Bembea alioimba na msanii mwenzake Aslay ambao mpaka leo mchana umefuatiliwa na watu milioni 1.61.
Wimbo wake wa Nishikilie umetafutwa na watu 557,000, Mwana (236,000) na zingine zikiwemo za Seduce Me (91,200) ambapo wimbo wa Bembea umempa asilimia 46 ya watazamaji wake kwa wiki hii.
Kimziki, Kiba amepata mafanikio kwa wimbo wake wa Mwana uliotazamwa mara milioni 18.9 ukifuatiwa na Seduce Me (milioni 11.4) na tatu bora ya msanii huyo inakamilishwa na wimbo wa Nagharamia (milioni 10.1) alioshirikiana na Christian Bella.
Alikiba amepata ya watazamaji milioni 3.43 kwa wiki hii waliofuatilia nyimbo zake. Picha| Mtandao.
4. Aslay
Mtanzania huyu alitambulishwa na wimbo wa Naenda kusema ambao aliimba miaka 8 iliyopita huku akijulikana kama “Dogo Aslay”. Kwa kipindi hicho, alifanya nyimbo na wasanii wakongwe akiwemo Temba na Banana Zoro.
Kimafanikio, Aslay anatamba na nyimbo ya Mhudumu (2017) ambayo imetazamwa mara milioni 12.1 ikifuatiwa na Natamba (2017) yenye kutazamwa na watu milioni 8.9 kwenye mtandao wa Youtube.
Katika chati ya YouTube wiki hii, Aslay ameshika nafasi ya tano kileleni huku akifuatiliwa na watazamaji 3.8.
Waliomfikisha Aslay nafasi ya tano ni watu kutoka nje ya Tanzania hasa Kenya iliyompatia wafuatiliaji milioni 1.4 pamoja na nchi zingine zikiwemo Marekani na Msumbiji.
Kwa Aslay, bila Tanzania, Kenya na Marekani asingeweza kuingia kwenye chati hii kwani zimtengenezea asilimia 88.6 ya wafuatiliaji wake wote wiki hii.
Zinazohusiana
3. Harmonize
Safari ya muziki ya kijana huyu ilianza mwaka 2015 baada ya kuachia ngoma yake ya kwanza ya Aiyola ambayo ni ya nne kati ya nyimbo zake zenye mafanikio.
Kwa wiki hii Harmonize anakaa kwenye nafasi ya nne baada ya kuwa na wafuatiliaji milioni 11.3.
Kati ya nyimbo zake zote alizowahi kutoa, Kwangwaru iliyotazamwa na watu milioni 51.7 aliyomshirikisha Diamond Platnumz ndiyo nyimbo pekee iliyompatia watazamaji wengi.
Kufunga tatu bora ya msanii huyo ni Bado akimshirikisha Platnumz na Happy birthday. Kwa mujibu wa chati za Youtube, Harmonize ameshuka nafasi mbili baada ya msanii Innos’B kupanda hadi nafasi ya kwanza kwa wiki hii.
Harmonize amesikilizwa zaidi nchini Kenya kwa watu milioni 3.6, Tanzania (milioni 3.2) na nchi zingine zikiwemo Marekani na Ufaransa.
Platnumz ameshikilia nafasi ya pili tangu wiki iliyopita huku akiwa na wafuatiliaji milioni 20.3 ambapo wengi wanatokea nchini Kenya ikifuatiwa na Tanzania, Ufaransa, Marekani na Uingereza.
Platnumz amefanikiwa zaidi kwenye nyimbo ya Nana iliyotoka miaka minne iliyopita aliyoimba na msanii wa Nigeria, Mr Flavor baada ya kupata watazamaji milioni 54 huku ikifuatiwa na African beauty aliyoimba na msanii Omarion ambayo hadi kufikia Septemba 17 2019, nyimbo hiyo ina watizamaji milioni 39.
Tatu bora ya msanii Platnumz inafungwa na wimbo wa Number one Remix aliomshirikisha Davido ambayo imetazamwa mara milioni 38.5 kufikia Septemba 17.
Innos’B mwenye miaka 22, amepata umuarufu nchini Tanzania na kuingia kwenye chati hiyo ya Youtube Agosti 18 mwaka huu ikiwa ni baada ya kutoa wimbo wa Yope aliomshrikisha Diamond Platnumz. Picha| Mtandao.
1. Innos’B
Innos’B ambaye ni mwanamuziki kutokea nchi ya Congo DRC ameshikilia rekodi kama msanii anayefuatiliwa zaidi nchini Tanzania kufikia leo saa 9:00 mchana, kwa mujibu wa taarifa za YouTube charts.
Msanii huyo mwenye miaka 22, amepata umuarufu nchini Tanzania na kuingia kwenye chati hiyo ya Youtube Agosti 18 mwaka huu ikiwa ni baada ya kutoa wimbo wa Yope aliomshrikisha Diamond Platnumz.
Innos’B amefanikiwa kushika namba moja kwenye orodha ya wasanii wanaofatiliwa nchini Tanzania kupitia mtandao huo baada ya kutokea namba 21 wiki iliyopita.
Mpaka mchana wa leo, msanii huyo amefuatiliwa na watu milion8.86 akiwa katika nafasi ya kwanza na kuwaacha nyuma wasanii wa Tanzania.
Ni dhahiri kuwa orodha hii imetawaliwa zaidi na wanamuziki wa kiume. Wanamuziki wa kike walioingia kwenye orodha ya kumi bora ni Nandy ambaye ameshika nafasi ya sita na Nora Fatehi (Canada) anayeshikilia nafasi ya nane.
Fatehi ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kumshirikisha Rayvanny kwenye wimbo wa Pepeta.
Latest