‘Infographics’ 10 bora tulizochapisha mwaka 2018

December 31, 2018 8:51 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Waandishi wa nukta.co.tz wamechagua vielelezo mbalimbali vya habari hasa za takwimu ambavyo vilitoa habari zilizojificha na kuwasaidia wasomaji kuelewa mambo kirahisi.
  • Ukiachana na changamoto zinazotukabili, kwa timu ya nukta.co.tz, 2018 ulikuwa ni mwaka wa kuishi ndoto ya kutoa habari na makala bora za uchambuzi.

Ni kama jana tu ilikuwa Januari Mosi 2018. Leo tunamaliza mwaka yaani siku 365. Kuna mengi yemafanyika katika maisha yetu: mafanikio lukuki na yenye kutia faraja na yale ya kukatisha tamaa.

Ukiachana na changamoto zinazotukabili, kwa timu ya nukta.co.tz, 2018 ulikuwa ni mwaka wa kuishi ndoto ya kutoa habari na makala bora za uchambuzi kuhusu biashara, uchumi, teknolojia, uvumbuzi kwa ujumla, takwimu, safari na maendeleo.

Licha ya kuwa tumezalisha mamia ya habari na vielelezo vya takwimu (infographics) mwaka huu ambazo kwa namna moja ama nyingine zimesaidia kubadilisha maisha ya watu na biashara zao, waandishi wa Nukta wamechagua infographics 10 bora zilizochapishwa mwaka 2018.

Baadhi ya infographics  hizi ziliandaliwa na wanafunzi waliokuwa katika mafunzo ya uandishi wa habari jambo linalotutia moyo kuwa siku moja uandishi wa habari mtandaoni Tanzania utakuwa ukitawaliwa na vijana wabunifu na wenye shauku ya kubadili tasnia ya habari.

10. Ni kweli ngoma ya Harmonise ‘Kwangwaru’ ni zaidi ya zote?

9. Nani ana hazina kubwa ya wafuasi Twitter Tanzania

​

8. Habari iliyojificha nyuma ya ukuaji wa huduma za posta

7. Fursa zilizopo kwenye uzalishaji wa kakao Tanzania

​

6. Serikali inavyozidi kukaza uzi ukusanyaji wa mapato

5. Ukweli kuhusu uzalishaji wa samaki nchini

4. Tunayoyafahamu kuhusu ajali ya MV Nyerere

3. Kuna mchango wowote wa mazao ya GMO katika kilimo?

2. Sababu zinazofanya ufuatilie mjadala wa bei ya korosho

1. Walimu wa Sayansi ni nusu tu ya mahitaji

Huenda hukufanikiwa kusoma infographics zote tulizozalisha mwaka 2018, lakini je unafikiri zote zilizoainishwa hapa zinafaa kuingia kwenye 10 bora mwaka 2018?

Maoni yako yatasaidia kuboresha kazi zetu mwaka 2019.

Tunakutakia Kheri ya Mwaka Mpya 2019 na endelea kusoma habari za Nukta kwa yanayokuhusu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV