Google yasheherekea siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki “asiyevaa viatu”

August 27, 2019 7:11 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni aliyekuwa Mwanamuziki wa Cape Verde, Cesária Évora maarufu kama “Barefoot Diva”  ambaye alipendelea kupanda jukwaani bila kuvaa viatu. 
  • Alisifika zaidi kwa kupanda jukwaani wakati akiimba bila kuvaa viatu.
  • Anaendelea kukumbukwa katika maeneo mbalimbali duniani.  

Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Google imeungana na watu wengine duniani kusherehekea siku ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mwanamuziki wa Cape Verde, Cesária Évora maarufu kama “Barefoot Diva” ambaye alipendelea kupanda jukwaani bila kuvaa viatu. 

Aliwahi kutamba na wimbo wa Cesaria iliompa umaarufu mwaka 1987 na ukaboresha mwaka 1995.

Kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiwasaidia watu kutafuta vitu mbalimbali mtandaoni, imeweka picha ya Evora na kiunganishi cha taarifa zake katika sehemu ya kutafutia vitu (browser) ili kumkumbuka mwanamuziki huyo. 

Évora alizaliwa tarehe kama ya leo Agosti 27, 1941 nchini  Cape Verde na kufariki Desemba 17, 2011 akiwa na umri wa miaka 70 baada ya kupata matatizo katika mfumo wa upumuaji. Alikuwa na watoto wawili Fernanda na Eduardo Evora.

Évora alianza safari yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kushawishiwa na rafiki yake ambapo alifahamika zaidi kama “Barefoot Diva” kwa sababu ya sifa yake ya kupanda jukwaani na kuimba bila ya kuvaa viatu. 

Kutokana na umahiri wake wa kuimba nyimbo zilizogusa maisha ya watu alifanikiwa kupata tuzo mbalimbali za kimataifa ikiwemo ya Grammy Awards.

Aliwahi kushiriki katika mashindano ya “Order of Prince Henry” yaliyoandaliwa maalum kumkumbuka Prince Henry wa Ureno. Tuzo yake ya mwisho ya Kora All African Music Awards aliipata mwaka 2010 kabla ya kuanza kupigania afya yake mpaka umauti ulipomkuta mwaka 2011. 


Zinazohusiana:


Urithi alioacha kwa dunia

Pamoja na kuwa mwanamuziki, aliwahi kuwa Balozi wa Programu ya Chakula ya Umoja wa Mataifa (WFP) ambapo alikuwa anatumia muziki wake kuwaunganisha watu na kuhakikisha watu wanapata chakula bora kwa ajili ya maendeleo. 

Mwaka 2003, picha yake iliwekwa kwenye stempu za Cape Verde na kutumia katika shughuli za posta. Pia sanamu yake ilitengenezwa na  kuwekwa katika uwanja wa ndege wa Eponymous katika mji wa Mindelo nchini humo. 

Sanamu ya Mwanamuziki “Barefoot Diva” iliyopo katika uwanja wa ndege wa Eponymous katika mji wa Mindelo nchini humo. Picha|Mtandao. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV