Google yaadhimisha miaka 21 ya kuzaliwa, wadau watoa neno

September 27, 2019 1:05 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampuni hiyo ya teknolojia ya Marekani ilizaliwa Septemba 27, 1998.
  • Inasifika zaidi kwa kutoa huduma ya watu kutafuta vitu mbalimbali mtandaoni. 
  • Wadau wa teknolojia Tanzania watoa neno kuhusu sherehe hiyo.

Kampuni ya Google leo inaungana na watumiaji wa huduma zake duniani kusheherekea miaka 21 ya kuzaliwa kwake, huku ikitajwa kuleta matokeo chanya katika ulimwengu wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Google ambayo chimbuko lake ni Marekani ilizaliwa Septemba 27, 1998 na hadi kufikia leo imeanzisha bidhaa mbalimbali ikiwemo barua pepe ya Gmail ambayo imekuwa kiungo muhimu cha upatikanaji wa bidhaa zake zingine. 

Bidhaa nyingine za kampuni hiyo ambazo zinapatika katika duka lake la mtandaoni la Play Store ni pamoja na Google docs, Google sheets & Google slides), Google mail, Google Calenders, Google drive, Google messaging na Video chat, Google translates, Google photos. 

Hata hivyo, inasifika zaidi kwa bidhaa mama ya ‘Google Search Engine’ inayotumika na watu wengi katika utafutaji wa vitu mbalimbali mtandaoni. 


Soma zaidi:  


Wakati Google ikisheherekea siku ya kuzaliwa, haitawasahau waanzilishi wake wawili Larry Page pamoja na Sergery Bin ambao walikuwa wanafunzi wanaochukua Shahada ya Uzamivu katika chuo cha Stanford huko Marekani. 

Kupitia bidhaa zake, kampuni hiyo imeweza kugusa maisha ya watu wengi na kuzisaidia taasisi na mashirika mbalimbali kutoa huduma kwa njia ya haraka na urahisi. 

Mtaalamu wa teknolojia kutoka kampuni ya Innovations Solutions, John Simbila anasema mchango wa Google ni mkubwa ulimwenguni kwa sababu ya bidhaa zake kutumika katika shughuli mbalimbali. 

“Kusheherekea siku kama ya leo ni muhimu kwa  dunia nzima kwani tunaona mchango mkubwa ambao kampuni hiyo ya teknolojia imetupa siyo tu wanateknolojia bali karibu dunia nzima,” amesema Simbila.

Kwa watumiaji wa simu zenye mfumo endeshi wa Android ndiyo wamekuwa wakifaidika na huduma za Google. 

Enable Notifications OK No thanks