Google Fusion Tables kuzikwa rasmi Desemba 3

September 12, 2019 6:09 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampuni ya teknolojia ya Google imesema ifikapo Desemba 3, 2019 itaifunga rasmi programu tumishi ya Google Fusion Tables iliyokuwa inatumiwa kuchambua data na kusanifu michoro mbalimbali.
  • Katika kipindi cha miezi mitatu iliyobaki, Google imewashauri watumiaji wa programu hiyo, kuamisha nyaraka na kazi zao ili kuepuka usumbufu wakati itakapoondolewa sokoni rasmi. 

Kampuni ya teknolojia ya Google imesema ifikapo Desemba 3, 2019 itaifunga rasmi programu tumishi ya Google Fusion Tables iliyokuwa inatumiwa kuchambua data na kusanifu michoro mbalimbali. 

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyobaki, Google imewashauri watumiaji wa programu hiyo, kuamisha nyaraka na kazi zao ili kuepuka usumbufu wakati itakapoondolewa sokoni rasmi. 

Hata hivyo, Google imetoa njia ya kuwasaidia wateja wake kwa kuwapatia zana (tool) ijulikanayo kama “Google Takeout” kwa ajili ya kuhamisha nyaraka zao ili zisipotee bila kujali wingi wake kwani imewekwa kirahisi kuzihamisha kupitia programu hiyo. 

Unaweza kuzirekodi hizo data kwa mifumo tofauti kati ikiwemo “JavaScript Object Notation” (JSON), “Comma-separated values” (CSV) na “Keyhole Markup Language” (KML).


Soma zaidi:  


Programu hii ilianzishwa Juni 9, 2009 na imekuwa ikitumika zaidi na Waandishi wa habari za takwimu kwa ajili ya kukusanya, kutengeneza na kutuma takwimu kwa njia ya mbalimbali ikiwemo majedwali.

Wakati wanafunga mifumo yote inayoingiliana na programu hiyo ifikapo tarehe husika ambapo watumiaji wote wataanza kuona jumbe (error message) katika data zote zitakazokuepo kwenye programu hiyo.

Kama Google itafanikiwa kuizika rasmi Google Fusion Tables basi ni itakuwa imeziondoa rasmi sokoni programu zake mbili katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuifuta Google Plus Februari 4, 2019.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nukta TV

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Nukta TV

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Nukta TV