Filamu ya ‘Terminator Dark Fate’ yamrudisha Anold Schwarzenegger uwanjani

November 1, 2019 12:32 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Amerudi kwenye chati hiyo akiwa na miaka 72 katika filamu ya “Terminator Dark Fate”.
  • Inasimulia kisa cha(Rev-9) roboti asiyekufa.

Baada ya Rambo kutamba na “Last Blood” huenda visu, mabomu na mitego yake ikasahaulika kwani Anold Schwarzenegger, amerudi kwa kasi.

Milipuko na ajali za ndege zinaibua sauti inayosema “Sitaki mtu afe tena kwa ajili yangu”. Sauti hiyo ni yake Dani Ramos (Natalia Reyes) ambaye alikuwa ni shabaha ya roboti asiyeangamizwa hata kwa risasi moja wala mlipuko wa petroli.

Roboti huyo mwenye muundo Rev-9 (Brett Azar) aliyejulikana kama Liquid terminator ambaye amewasili kutoka nyakati zijazo (the future) na amekuja kwa ajili ya kazi moja tu! Nayo ni kumuua Ramos.

Mambo yanazidi kuchanganya pale mwanadada  Grace (Mackenzie Davis) ambaye pia ana uroboti na ametoka kule kule (Nyakati zijazo) kwa ajili ya kumlinda Ramos.


Zinazohusiana


Hata hivyo, maji yanawafikia shingoni na ndipo wanapoungana na Sarah Connor, na T-800 (Arnold Schwarzenegger(72)) kwa ajili ya kukabiliana na Rev-9.

Hakika unahitaji kufuatilia mkasa huu uliogharimu takribani Sh461.1 bilioni  chini ya kiongozi Tim Miller ambaye filamu ya Dead Pool pia ni kazi ya mikono yake.

Ni nani atauliwa na Rev-9; roboti ambaye kifo kinamkimbia kila saa? Jibu swali hilo kwa gharama ya Sh10,000 tu kupitia kumbi za kuangalizia  sinema za Mlimani City, Aura Mall na zinginezo.

Kama siyo mpenzi wa filamu za vita, Basi Maleficent na Gemini Man bado zipo kwenye kumbi hizo. Hustahili kukosa burudani.

Enable Notifications OK No thanks