Filamu hizi zinavyofundisha uvumilivu katika kazi, maisha

August 30, 2019 9:51 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Zimeanza kuonyeshwa kwenye kumbi za kutazamia filamu kwa siku sita zijazo
  • Zimesheheni mafundisho mengi ikiwemo uvumilivu

Dar es Salaam. Baada ya siku tano mfululizo za kazi, unastahili mapumziko ambayo yatachangamsha mwili na akili yako. 

Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao sehemu ya mapumziko yao inahusisha kutazama filamu, basi usiache kuangalia filamu hizi za Magharibi ambazo zinaonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye kumbi za kuangalizia filamu zikiwemo Dar Free Market (DFM) na Mlimani City kwa jiji la Dar es Salaam.

Blinded by the light

Javek Khan(Viveik Kalra) ana ndoto za kuwa mwandishi mzuri hapo mbeleni lakini familia yake ambayo imeshikilia ukale, inamtaka kuwa zaidi. Baada ya kwenda masomoni, anakutana na marafiki wanaomkutanisha na nyimbo za Bruce Springsteen na baada ya kuzisikiliza anasema, “Hizi nyimbo, zinaniongelea mimi”. 

Familia yake ya kihindi itasemaje? na Je, atamaliza masomo? Majibu ya maswali hayo yatapatikana iwapo utapata fursa ya kufuatilia filamu hii iliyogharimu takribani Sh34.5 bilioni ambayo imepata mshawasha kutoka kwenye  maisha halisi ya mwandishi wa Uingereza Sarfraz Manzoor (48). 

Filamu hiyo imesimamiwa na kiongozi Gurinder Chadha (59) akihusisha manguli kwenye uigizaji wakiwemo Hayley Atwell ambaye ni mshiriki kwenye filamu ya muendelezo ya The Dutchess ya mwaka 2008 na Rob Brydon (54) ambaye ni mwanamuziki, muigiza sauti na mchekeshaji.

Filamu ya Blinded bythelight ina mchanganyiko wa waigizaji wakihindi na wakiingereza. Picha| Mtandao


Zinazohusiana

Filamu za kimataifa zitakazoingia sokoni mwishoni mwa 2019


47 Meters down uncaged

Pale binti anavyoshawishika kukataa kutalii na wazazi wake na badala yake kwenda na marafiki zake kwenye sehemu isiyotembelewa na watu wengi, inamuachia historia ambayo hawezi kuisahau.

Furaha anayoipata mwanzoni inamsahaulisha shida za dunia lakini mambo yanabadilika pale papa wanapoanza kuchafua maji kwa damu isiyo ya mnyama wa baharini. 

Watafanyaje ikiwa wao pekee ndio viumbe wageni kwenye maji hayo? Fuatilia kujua namna Sh27.6 bilioni imetumika kuwezesha kazi hii iliyosimamiwa na Johannes Roberts (43) ambaye ni kichwa nyuma ya “Road Kill” na “The Strangers” akiwa na waigizaji machachari kama Sophie Nélisse (Close 2019 & The book Thief 2013), John Corbett (Sex and the city & My big fat greek wedding) na Khylin Rhambo (Teen Wolf & Ender’s game).

kukataa kutalii pamoja na wazazi wake, inakua moja kati ya maamuzi anayojutia. picha| mtandao

Kama ulipitwa na filamu za wiki iliyopita, bado una muda kwani filamu kama Lion king, Angel has fallen na Fast and furious (Hobbs and Shaw) bado zinaonyeshwa. 

Bado unatafuta kitu cha kufanya wikiendi kujipumzisha na uchovu wa kazi za wiki nzima?

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV