FCC yapewa kibarua kuwalinda watumiaji wa huduma za kifedha mtandaoni

March 15, 2022 11:39 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Yatakiwa kutengeza mfumo imara wa kuzuia wizi wa kimtandao.

Mwanza. Serikali  imeiagiza Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) kufanya utafiti ili kupata mifumo bora ya kuzuia wizi wa fedha kwa njia ya mtandao hapa nchini.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji aliyekuwa akizungumza katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Kumlinda Mtumiaji Duniani jijini Mwanza leo Machi 15, 2022 amesema bado jamii inasumbuliwa na ulaghai na wizi wa kimtandao na kwamba FCC kwa kushirikiana na vyombo vingine wafanye utafiti wa kina ili kukabiliana na janga hilo la kitaifa na kidunia.

Amesema ili watu wawe salama katika utumiaji wa huduma za mtandaoni hasa za kifedha wainapaswa kufuata mifumo imara iliyowekwa na Serikali.

Aidha, Waziri huyo amewataka watoa huduma za fedha wote kuweka mifumo itakayolinda watumiaji ambao ni wateja wao.

Kuhusu masuala ya ukatatishaji fedha pamoja na ugaidi duniani yanayofanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa,  vyombo vilivyopewa dhamana kusimamia sheria vinatakiwa kuliona hilo na kuliwekea misingi imara ya kupambana nalo.

“Utakatishaji wa fedha unaharibu kabisa uchumi wa nchi na suala hili ni lazima kama nchi tupambane nalo ili kulimaliza katika jamii yetu,”  amesema Dk Kijaji.

Amepongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuendelea kuwa na mifumo imara ya kulinda watoa huduma za fedha wa ndani na nje nchi.

Ifikapo mwaka 2024 inakadiriwa kuwa watu bilioni 3.6 duniani kati ya bilioni 7 watakuwa wanatumia huduma za fedha kwa njia ya kidigitali, hivyo ulinzi wao ni muhimu ili kuendelea kufaidika na fursa za kidijitali.  

Mwenyekiti wa bodi ya FCC, Dk Agrey Mlimuka amesema, wataendelea kusimamia haki katika ushindani ya kibiasahara nchini.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

Nukta TV

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Nukta TV