Faida utakazopata ukitumia ‘milkshake’ ya embe

January 13, 2023 8:55 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kinywaji hiki ni chanzo kizuri cha vitamini C, protini na madini chuma.
  • Kinafaa kutumiwa na watu wa rika zote.
  • IIi kuitengeneza utahitaji blenda yenye uwezo wa kusaga vitu vigumu.

Dar es Salaam. Juisi za matunda ni moja ya kinywaji kizuri kinachoweza kutumiwa wakati wote na watu wa rika zote isipokuwa wale wenye mzio na changamoto nyingine za kiafya.

Uzuri wa juisi hizi unaweza kutengeneza nyumbani kwa gharama ndogo ukilinganisha na juisi za viwandani ama vinywaji vingine.

Kabla ya msimu wa maembe haujaisha tutengeneze milkshake ya embe (juisi yenye mchanganyiko wa maziwa na embe) yenye faida nyingi mwilini ikiwemo madini ya chuma, protini na vitamin C.

Fuatana nami kujifunza namna ya kuandaa kinywaji hiki pendwa chenye ladha ya kipekee.

Maandalizi

Osha embe, (maembe) menya na ukatekate vipande vidogo vidogo vitakavyoweza kusagika kwa haraka.

Andaa blenda, weka matunda yako, kikombe kimoja cha maziwa, vipande vya barafu na aina yoyote ya ladha unayopendelea kisha usage mpaka matunda yalainike.

Hakikisha blenda unayotumia iwe yenye uwezo wa kusaga vitu vigumu (heavy duty blender) ili kurahisisha mchakato wa matunda kusagika.

Ikiwa unatumia blenda ya kawaida utalazimika kurudia kusaga mara mbili au zaidi ili maembe yasagike vizuri kwa sababu aina hii  ya juisi haichujwi.

Ukishamaliza kusaga unaweza kuweka juisi yako kwenye friji ili ipate baridi zaidi au kuweka kwenye glasi tayari kwa kunywa.

Haina haja ya kuongeza sukari. Embe lina sukari ya kutosha kukuwezesha kufurahia kinywaji hicho.

Unaweza kuongeza urembo wa vipande kadhaa vya embe, au jani la mnanaa (mint) juu ya glasi ili kuongeza muonekano mzuri.


Tangazo

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV