Fahamu faida za mazao ya mikunde kiafya

February 11, 2024 2:28 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kuimarisha afya ya binadamu pamoja na mazingira.
  • FAO yabainisha kuwa mikunde inaweza kumuepusha mlaji na magonjwa moyo na kansa.

Mikunde ni miongoni mwa makundi ya chakula ambayo hujumuisha mazao ya chakula kama maharage,choroko, mbaazi, kunde na njegere.

Je unazifahamu faida za kiafya za kula mazao ya mikunde?

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) linaeleza kuwa ulaji wa aina hii ya chakula unaweza kuimarisha afya ya binadamu, mifugo pamoja na udongo kutokana na wingi wa virutubisho vilivyopo..

“Kwa wastani, kunde huwa na asilimia 19 hadi 25 ya protini, huku nyinginze zikizidi asilimia 30 ya protini…zao hili ni muhimu kwa watu ambao lishe zao hazihusishi ulaji wa nyama,” imesema taarifa ya FAO iliyochapishwa Februari 10, 2024.

Mbali na faida hizo,FAO inaeleza mikunde huweza kumuepusha mlaji na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na magonjwa ya moyo kutokana na  zao hilo kuwa na kiwango kidogo cha mafuta na chumvi. 

Mazao ya mikunde huweza kupikwa kwa aina mbalimbali ambayo inaweza kumvutia mlaji na kuipatia faida za kiafya.Picha|Mapishi Mix.

Mazao hayo pia husaidia kutunza mazingira kutokana na uwezo wake wa kuzalisha hewa ya nitrojeni ambayo inarutubisha ardhi, pia aina nyingi za mikunde huvumilia ukame, hivyo kuzalisha chakula hususan katika jamii zinazopata mvua chache.

Kwa upande wa Tanzania, ripoti ya hali ya chakula kwa mwaka 2020/2021 na 2021/2022 inayotolewa na Wizara Ya Kilimo inabainisha kuwa mwaka 2021/2022, tani 2.1 za mikunde zilizalishwa sawa na  asilimia 11.6 ya chakula chote kilichozalishwa nchini.

Kutokana na takwimu hizo,Tanzania ina ziada ya tani 1.2 ya zao la mikunde itakayotosha kwa matumizi na kuwahakikishia watanzania faida lukuki ikiwemo virutubisho vinavyoimarisha mwili. 

Hata hivyo, FAO  inasema pamoja na faida zote hizo, mikunde imepoteza umaarufu wake katika miaka ya karibuni na matumizi yake duniani kote yamepungua kwa sababu ya ongezeko la kipato miongoni mwa walaji na pia walaji kupendelea vyakula vingine zaidi ya mikunde.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV