Facebook kuzuia matangazo ya ‘uponyaji wa miujiza’ mtandaoni
- Tayari imeboresha mifumo yake kuhakikisha matangazo hayo hayawafikii watumiaji wake.
- Hatua hiyo ni kuwalinda watumiaji wake dhidi ya matangazo ya afya yanayopotosha.
- Miongoni mwa matangazo hayo ni yale ya kupunguza uzito.
Katika kuhakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya habari za uzushi, Facebook imesema itaondoa matangazo ya ‘uponyaji wa miujiza’ na afya yanayopotosha ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa mtandao huo.
Baadhi ya watumiaji wamekuwa na malalamiko kuwa wanapata matangazo hayo yenye kutoa jumbe za kutoa suluhisho la afya zao bila ridhaa katika kurasa zao.
Baadhi ya matangazo hayo ni yale yanayohamasisha kupungua kwa uzito (weight loss cures) kwa nguvu za miujiza pasipo kuzingatia taratibu za kiafya.
Facebok imeeleza kupitia taarifa yake, kuwa mwezi uliopita wamefanya mabadiliko mawili ya kimfumo ili kupunguza kuonekana kwa taarifa zinazokuza au kuogopesha kuhusu masuala ya afya pamoja na matangazo yanayohusiana na bidhaa za afya hasa zile zinazotumia nguvu za miujiza.
Facebook imesema inawajibika kufanya hivyo ili kuwawezesha watumiaji wake kupata taarifa au matangazo sahihi na siyo yale ya uponyaji wa kimuujiza (miracle cure) wala taarifa za mtangazo ya afya yanayohusisha matibabu au vidonge vya kupunguza uzito.
Zinazohusiana:
- Zawadi ya Mark Zukerberg: Facebook kuwakutanisha makapela mtandaoni
- Facebook yafanya maboresho utafutaji wa bidhaa mtandaoni
Kuboreshwa kuwa mifumo hiyo ya taarifa, huenda kukawasaidia watumiaji wa Facebook zaidi ya bilioni 2 kukabiliana na habari za uongo hasa zile zinazoathiri afya zao.
Jinsi mtandao wa facebook unavyopambana na taarifa hizo
Facebook imesema utaondoa matangazo hayo kwa kuangalia maneno yanayotumiwa mara kwa mara kwenye matangazo hayo na kisha kuiwezesha mifumo iliyoboreshwa kutokuruhusu matangazo ya aina hiyo kuonekana kwa watumiaji wake.
Mtandao huo ambao unamilikiwa na raia wa Marekani, Mark Zuckerberg umekuwa sehemu muhimu kwa wafanyabiashara kutangaza huduma na biadhaa wanazotoa mtandaoni.
Hata hivyo, baadhi ya watu wasio na nia njia njema wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuwatapeli watu na kuwauzia bidhaa ambazo hazijakidhi viwango vya ubora unaohitajika kuwepo sokoni.
Mfano wa matangazo ambayo yanaweza kuondolewa katika ukurasa wa Facebook. Picha|Mtandao.
Latest
