CHATI YA SIKU: Asilimia 9.1 ya Watanzania wana kisukari

November 16, 2018 11:30 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali imesema kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri kati ya miaka 25 hadi 64 wana kisukari.
  • Hiyo ni sawa na kusema kati ya watanzania 100 waliopo nchini 9 wanaugua ugonjwa huo hatari kwa sasa. 
  • Lengo la Serikali ni kupunguza wagonjwa wa kisukari kwa asilimia 28 ifikapo 2025 sambamba na kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa huo ambao hugharimu pia fedha nyingi kuutibu.

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine duniani leo Novemba 14, 2018 kuadhimisha Siku ya Kisukari Duniani (World Diabetes Day), takwimu zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa kisukari mwaka hadi mwaka duniani kote. 

Tamko la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu lilitolewa leo kuadhimisha siku hiyo limeeleza kuwa Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa idadi ya watu wenye kisukari imeongezeka kutoka milioni 108 mwaka 1980 hadi kufikia milioni 422 mwaka 2014. 

Inakadiriwa kuwa kama hakutakuwa na juhudi za makusudi za kupambana na ugonjwa huu, ifikapo mwaka 2035 kutakuwa na wagonjwa 592 millioni duniani.

Kwa upande wa Tanzania, utafiti wa STEPS uliofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikianana Taasisi ya utafiti wa mgonjwa ya binaadamu (NIMR), na Shirika la Afya Duniani, mwaka 2012 uliohusisha wilaya 50 nchini Tanzania, unaonesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri kati ya miaka 25 hadi 64 wana ugonjwa wa kisukari.


Zinazohusiana:


Serikali kupitia Wizara ya Afya inatumia maadhimisho haya kama sehemu ya kuhamasisha jamii kushiriki katika kudhibiti ugonjwa wa kisukari. 

“Lengo letu ni kupunguza wagonjwa wa kisukari kwa asilimia 28 ifikapo 2025. Sambamba na kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa kisukari, lengo la Serikali ni kuhakikisha tunapanua huduma za kupima na matibabu,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka 2018 ni “Familia na kisukari”.  

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV