CAG: Dawasa ilikusanya mamilioni bila kusoma mita za maji

March 30, 2022 2:27 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Sh755.65 milioni zilikusanywa na mamlaka hiyo
  • CAG asema hali hiyo inaweza kuifanya Dawasa kubambikiza ankara au kukusanya mapato pungufu. 
  • Mifumo ya kiteknolojia ya ulipaji ankara za maji yaanzishwa kumaliza tatizo hilo.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekuwa ni moja kati ya mamlaka zilizoanikwa mapungufu yake na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2020/21 kutokana na udhaifu katika usomaji mita za maji. 

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere amemweleza Rais Samia Suluhu Hassan leo Machi 30 jijini Dodoma kuwa Dawasa ilitoza bili za maji kwa wateja 1,207 na kukusanya Sh755.65 milioni bila kusoma mita za maji kwa matumizi ya maji ya kila mwezi.

Kati ya idadi hiyo wateja 371 walikuwa na mita mbovu huku 836 wakitozwa huduma za maji taka bila kuwa na taarifa sahihi zinazotumika kukadiria gharama za maji taka.

“Utaratibu huu Mheshimiwa Rais unaweza kusababisha wateja kulipa zaidi au pungufu ya kiasi kilichotakiwa,” amesema Kichere.

Wateja wa Dawasa kwa nyakati tofauti wamekuwa wakilalamikia uwepo wa ankara za maji zisizokuwa na uhalisia. 


Zinazohusiana:

Katika kutatua changamoto hiyo, Rais Samia Suluhu amesema kuwa kuna mifumo mipya ya kiteknolojia ya ulipaji bili za maji imeanzishwa ili kuboresha huduma za ulipaji wa bili hizo.

Mifumo hiyo, Rais Samia amesema itamuunganisha mteja moja kwa moja na zitamuwezesha kuhakikisha kama bili atakayotumiwaa ni sahihi au la.

“ Siku ya maji tuliyoifanya 22 mwezi huu (Machi) kuna systems (mifumo) mpya zimeanzishwa kuna Maji App lakini kuna ‘unified water bills’ (Mjumuisho wa bili za maji) ambako sasa bili sasa zitatoka kwa kutumia Tehama na sidhani kama kutakuwa na human control au kupeleka bili ambazo mita hazikusomwa,” Rais Samia. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV