‘Boxing Day’: Zifahamu zawadi 8 za kumpatia umpendaye

December 26, 2024 8:00 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Mnunulie saa, manukato, simu na hata gari.
  • Zawadi kubwa kuliko zote ni kumpatia muda wako akufaidi. 

Dar es Salaam. Siku ya ‘Boxing Day’ ni siku inayosherehekewa baada ya Krismasi. Ni siku ya kufungua na kupeana zawadi. Watu hutoa zawadi kwa wapendwa wao, familia, na hata watu wasio na uwezo kama ishara ya shukrani na upendo.

Zawadi zinazoweza kutolewa siku hii ziko za aina tofauti lakini hutegemea zaidi uhusiano wa mtu na mtu na hali ya kifedha ya mtoaji. 

Kama bado unawaza ni zawadi gani umpatie umpendaye, Nukta Habari tumekuandalia baadhi ya zawadi ambazo unaweza kumpa mtu wako wa karibu:  

  1. Saa ya mkononi

Endapo unahitaji kumpa mtu zawadi awe, baba, kaka, mume au mpenzi saa ya mkononi itakuwa zawadi nzuri kwao kwani kila muda watakaokuwa wanatazama muda basi nyonyo zao zitajaa kumbukizi zako.

Zawadi ya saa ina umuhimu mkubwa kwa mpokeaji kwa sababu inachanganya matumizi ya kivitendo, maana ya kihisia, na alama ya heshima. Picha/ Kupatana.

Zawadi hii imependekezwa na Alex Juma, mkazi wa jiji la Dar es Salaam ambaye amesema kuwa saa ya mkoni kwake ni zawadi bora ya kutunza kumbukizi za mtu aliyempa.

Kumpa mtu saa inaweza kuwa ni ishara ya kuthamini muda au kutamani awe na maisha yenye mpangilio.

  1. Manukato

Zawadi hii haichagui jinsia anaweza kupewa mtu yoyote na bado ikamfaa. Jambo la kuzingatia ni aina ya manukato anayopewa mtu wa jinsia ya kike na jinsia ya kiume.

Manukato yanayotoa harufu nzuri huashiria upendo, heshima, au shukrani. Manukato yanaweza kuwa mafuta ya kupaka mwilini au pafyumu.

Unapochagua harufu itakayodumu siku nzima, kuelewa aina tofauti za harufu ni jambo la msingi.Picha /perfume.comBlog.

Manukato yanaweza kuonyesha kujali kwa mtoaji, kwani mara nyingi huchaguliwa kwa kuzingatia tabia ya mpokeaji. Zawadi ya manukato pia inaweza kuwa na maana ya kumtakia mtu uzoefu mzuri au wa kuvutia, kwani harufu nzuri mara nyingi huchangia kujisikia vizuri na kujiamini.

Manukato hutengeneza kumbukumbu nzuri kwa mtu aliyepewa kwani kila atakapotumia hurejesha hisia kwa mpendwa wake aliyemzawadia.

  1. Ice cream na chokoleti 

Bidhaa hizi za chakula zimekuwa zikipendwa na watu wengi kama kiburudisho na kuimarisha afya. Kama mtu wako wa karibu anapendelea chokoleti na ice cream basi, msimu huu ndio wakati mzuri wa ‘kushow love kwake. 

Zawadi za chocolate na ice cream zina umuhimu mkubwa katika tamaduni nyingi na maisha ya kila siku, hasa kutokana na furaha na hisia nzuri ambazo huleta kwa wapozi, familia, na marafiki. Picha / Times Food.

Mnunulie bidhaa hizo za kutosha ili akatunze kwenye friji yake na kuzitumkia taratibu. 

  1. Pochi na urembo wa kike

Ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu anapenda kupendeza, zawadi hizi zinapendelewa zaidi na watoto wa kike awe mkubwa au mdogo.

Hivyo ukimununulia pochi na urembo kama heleni, mikufu ya shingoni, vipuli na urembo wa nywele vitamfanya mtu kujiona kuwa anathamani zaidi.

Pochi ni moja ya vifaa muhimu vinavyohusishwa na mtindo wa maisha wa wanawake wengi. Picha/ Jiji Tanzania.

Kuna wengine utawaona kila akitaka kutoka amejitupia vitu hivyo, sio kwa kuwa hana vingine ni kwa sababu kila mara humfanya ajihisi wa thamani kwa mtu aliyemletea.

Chunguza aina ya pochi au urembo anaopenda mpenzi wako na mnunulie ili ikifungua boksi akutane na surprise 

  1. Zawadi ya nguo

Zawadi ya nguo ina maana ya kumpa mtu vazi kama sehemu ya kuonyesha upendo, shukrani au heshima.

Nguo inaweza kuwa shati, gauni au mavazi mengine kulingana na aina ya mtu.

Zawadi ya nguo ina umuhimu mkubwa katika maisha ya mpokeaji kwa njia mbalimbali, zikiwemo za kihisia, kiutamaduni, na kivitendo. Hapa kuna baadhi ya sababu kuu za umuhimu wa zawadi ya nguo. Picha/ Gat Fashion Lab.

Neema Juma, mkazi wa Tanga anasema kuwa hakuna kitu kinamkosha kama akipata fursa ya kuvaa nguo mpya ambayo hajatoa pesa yake kununua.

Hakuna raha inayotawala moyo wa mtu kama kupata zawadi ya nguo adimu kutoka kwa watu wao wa karibu. 

  1. Simu mpya

Kwa wale wenye kipato kizuri, na wanaopenda kuwa tofauti na wengine hupendelea kununua simu na kuwapa wanaowapenda. Zawadi hubeba ujumbe mkubwa mmoja tu kuwa mawasiliano ni muhimu.

Hii inaweza kuwa msaada mkubwa kwa wapokeaji wa zawadi, hasa wanafunzi au wafanyakazi wanaotumia simu kwa kazi za kila siku. Picha/ Mobilecity.

Zawadi kama hizi mara nyingi hupendelewa na watu maarufu ambao kila wanapopewa zawadi huja kwenye mitando ya kijamii na kuonesha watu zawadi walizopewa.

  1. Chombo cha usafiri

Chombo cha usafiri kama gari, pikipiki au Bajaji ni moja ya zawadi ambayo huacha msisimko wa aina yake kwa mtu anayeipokea ikiwemo kilio.

Kama mtu wako wa karibu ana uhitaji wa gari mnunulie kwa sababu utakuwa umemrahisishia kupanda daladala na akwa huru kwenye gari yake huku akiokoa muda katika shughuli zake za kila siku.

Gari kama zawadi linatoa suluhisho kwa changamoto za usafiri. Mpokeaji anaweza kusafiri kwa urahisi kwenda kazini, shuleni, au kwenye shughuli za kila siku bila utegemezi wa usafiri wa umma. Picha/ istock.

Unaweza kununua pikipiki au Bajaji na kumpa kijana wako ili afanye biashara na aongeze mapato mwaka 2025 yatakayoboresha maisha yake.

  1. Zawadi ya muda

Huenda ukaona hii sio zawadi kwa hali ya kawaida. Ikiwa wewe ni mume au mke kila siku unafanya kazi itapendeza zaidi kumpa mwenza wako zawadi ya muda siku ya boxing day na hii itaongeza ukaribu kati yenu na kudumisha mapenzi zaidi.

Yohana Maxmillan, mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam yeye amebainisha kuwa zawadi kubwa anayoitaka siku ya boxing day ni kupata muda wa kuwa na mtu anayempenda sehemu tulivu na itakuwa ni zawadi kubwa sana kwake.

Hizi ni baadhi ya zawadi unazoweza kumpatia umpendae. Ongeza zawadi zingine katika comment hapo chini ili wengine nao wajipatie maujanja ya kuwafurahisha wawapendao. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks