Bei ya ngano bado mtihani Lindi
August 30, 2024 7:23 pm ·
Hemed Suleman
Share
Tweet
Copy Link
Ili ununue gunia moja la ngano la kilo 100 mkoani Lindi utalazimika kulipa Sh400,000 ikiwa ndiyo bei ya juu zaidi kurekodiwa nchini Agosti 30 mwaka huu.
Bei ya juu ya ngano Lindi ni mara sita zaidi ya ile iliyotumika mkoani Rukwa ya Sh65,000 kwa gunia la kilo 100 la bidhaa hiyo muhimu katika kuandaa vitafunwa kama maandazi, chapati na mikate.
Wakati Lindi wakilia na ngano, wakazi wa Dar es Salaam wanaendelea kuvunja vibubu baada ya gunia la kilo 100 la maharage kuuzwa kwa bei ya juu katika jiji la Dar es Salaam kwa Sh390,000, karibia mara mbili ya bei ya chini iliyorekodiwa Arusha ambayo ni Sh160,000.
Latest
13 hours ago
·
Lucy Samson
Sababu Mbowe kugombea tena uenyekiti Chadema
16 hours ago
·
Lucy Samson
Mbowe kugombea tena uenyekiti Chadema
1 day ago
·
Davis Matambo
Majaliwa akabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa mafuriko Hanang
2 days ago
·
Kelvin Makwinya
Viwango vya kubadili fedha za kigeni leo Disemba 20,2024