Ad Astra: Filamu nyingine ya kutazama wiki hii

September 20, 2019 10:05 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Filamu hiyo ni  Ad Astra iliyogharimu Sh229.8bilioni itaonyeshwa katika kumbi mbalimbali za sinema wiki nzima kuanzia leo.
  • Ikiongozwa na James Gray, kijana Roy McBride (Brad Pitt) anatakiwa kwenda angani kutatua changamoto za mradi wa kielektroniki. 
  • McBride ataweza kupingana na baba yake kuokoa dunia?, safari yake ni kama kujitoa kafara. Ataweza kuiacha familia yake?

Dar es Salaam. Unasababu nyingi za kukaa kwenye kiti cha kumbi ya sinema, kuweka mkono wako kwenye pembe moja ya kiti chako huku mkono mwingine ukitafuta bisi kwenye mfuko wa kilaji hicho ili kuburudika na filamu mpya iliyoingia sokoni wiki hii. 

Filamu hiyo ni  Ad Astra iliyogharimu Sh229.8bilioni itaonyeshwa katika kumbi mbalimbali za sinema wiki nzima kuanzia leo.

Ikiongozwa na James Gray, mkasa tungwa “fictional” wa kijana Roy McBride (Brad Pitt) anatakiwa kwenda angani kutatua changamoto za mradi wa “Power surge” ulioanzishwa na baba yake kwa ajili ya kufanya tafiti ya masuala ya angani.

Akiwa na waigizaji wenzake  Ruth Negga na Tonny Lee, McBride ameishi miaka mingi akijua baba yake (Tonny Lee) amefariki lakini anabaki mdomo wazi pale anapopata taarifa ya kuwa huenda baba yake yupo hai.

Akiwa hajapona baada ya kupata ajali, McBride anatakiwa kuzuia mradi wa “Power Surge” kwani unahatarisha usalama wa ulimwengu mzima.


Zinazohusiana


Safari ya kuzuia mradi huo ni ngumu kwani sio rahisi kukabiriana na baba yake ambaye mbali ya kuwa mzazi wake ni motisha kwenye utendaji wa kazi zake.

Je McBride ataweza kupingana na baba yake kuokoa dunia?, safari yake ni kama kujitoa kafara. Ataweza kuiacha familia yake?

Maswali hayo utayajibu baada ya kulipia Sh10,000 siku yoyote ila Alhamisi ambayo utalipia Sh5000 kuitazama filamu hiyo kwenye kumbi uipendayo Jijini Dar es Salaam.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV