Urembo wa kucha unavyowaweka matatani wanawake -3

August 13, 2021 6:05 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanaotaka urembo wa kucha watakiwa kupata huduma hizo kwa wataalam.
  • Wakumbusha kutumia kucha bandia au rangi kama kuna ulazima.

Dar es Salaam. Katika makala mbili zilizopita tuliangazia kwa undani madhara ya rangi za kucha na matumizi yasiyofaa ya kucha bandia na visababishi vyake.

Madhara hayo ni pamoja kuoza na kubanduka kwa kucha, maumivu, kukatika na kubadilika rangi ya asili ya kucha. 

Wengine wako katika hatari ya kupata saratani kutokana na kemikali zilizopo kwenye rangi na dawa zinazotumika kukausha rangi inapokuwa imepakwa kwa kucha.

Ili kuhakikisha urembo huo hauthiri afya za wanawake ambao ndiyo walengwa wakuu, yapo mambo ya kuzingatia kwa watoa huduma na watumiaji yatakayowasaidia kuepuka madhara hayo.

Mtaalamu wa kucha mwenye uzoefu wa miaka mitatu, Gabriella Denho anasema changamoto ya kucha kuharibika, kuoza na kubadilika rangi zipo na amesikia na kuzishuhudia pia. 

Mtaalamu huyo ambaye humfuata mteja wake popote alipo, anasema kwa changamoto ya kuoza kucha, mara nyingi inasababishwa na kubandika kucha bila kufuata utaalamu ikizingatiwa kuwa baadhi ya wanawake hukaa na bidhaa hizo muda mrefu.

Changamoto inatokea pale taratibu za kubandika kucha hizo zinapokosewa na watu kufanya watakavyo, jambo linalowaacha na majuto yasiyo na majibu.

“Gundi aina ya “superglue” siyo gundi ya kucha lakini wapo watu wanaotumia superglue kubandikia wateja wao kucha. Ni vitu vidogo vidogo ambavyo vinawasumbua watu,” anasema Denho, mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Kabla ya mtu kupandikwa kucha au kupakwa rangi, kucha zake zinatakiwa zisafishwe vizuri, kuondoa rangi ya zamani na kuzikata kucha kulingana na mtu anavyopendelea.

Rangi ya kucha inakupa muonekano mzuri lakini usipokuwa makini urembo huo unaweza kukuletea madhara ya kiafya kama hautozingatia taratibu za kupaka. Picha| Today Show.

Usafi wa vifaa

Katika matengenezo ya kucha, kuna vifaa kama taulo, visu vya kuchongea kucha, mafuta na vibao vya kusugulia miguu, hivyo ni vema usafi ukazingatiwe ili kuwaepusha watu magonja na kuharibika kwa kucha.

Mjasiriamali wa juisi kutoka mgahawa wa Gracing Daily, Glory Mushi amesema kuchangia vifa pia ni kitu kinachotakiwa kutokupuuziwa.

Mwanadada huyo anasema ni vigumu kujua changamoto za ngozi alizo nazo mtu mwingine hivyo pale ni vema kila mteja atumie vifaa vyake.

“Nashauri kama una uwezo wa kifedha, nenda dukani nunua bidhaa zako ambazo hazipaswi kuchangia kama taulo na vile visu. Siku ya kwenda unaenda navyo, ukirudi nyumbani visu unaweza kuvichemsha au kuvitakasa. Unakuwa na uhakikia na usafi wako,” anasema Mushi.

Wataalam hao wanapendekeza kuwa watu wapate huduma za kucha kwa watu waliobobea ili kuepuka madhara.


TANGAZO


‘Punguzeni kasi’

Mtaalamu wa afya kutoka Hospitali ya Tarime iliyopo Mkoani Mara, Dk Reinfreed Haule  anashauri wanawake wapunguze matumizi ya kucha bandia au kupaka rangi mara kwa mara na wafanye hivyo kama kuna ulazima.

Anasema bidhaa za urembo wa kucha zina kemikali ambazo mtu hawezi kukwepa madhara yake yawe ya muda mfupi au muda mrefu.

“Kuna rangi nyingi tu za asilia ambazo Mungu ametupa, tumekuwa tukiwaona mama zetu wakijipamba kwa hina zinazotokana na mimea na changamoto hizo kwao hazikuwepo kama ilivyo sasa,” anasema Dk Haule.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks