Rais Samia: Acheni Urasimu tutekeleze miradi kwa wakati

February 14, 2023 12:54 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Akemea fitina za wakandarasi pamoja na ucheleweshaji wa vibali vya ajira.
  • Asisitiza kasi katika utekeleaji wa miradi ili wananchi wapate maendeleo.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitaka taasisi za Serikali au binafsi pamoja na mashirika kuacha urasimu katika utekelezaji wa miradi ya umeme, jambo litakaloongeza kasi ya kukamilika kwake na kuboresha maisha ya Watanzania.

Ris Samia aliyekuwa akishudia hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mahsusi ya umeme leo Februari 14, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam amewaambia wahudhuriaji kuwa, urasimu ni miongoni mwa changamoto inayofanya miradi kutokamilika kwa wakati.

Kwa mujibu wa Rais Samia miongoni mwa mambo ambayo hukumbwa na urasimu katika utekelezaji wa miradi ya umeme ni pamoja na uchaguzi wa wakandarasi, utoaji wa vibali vya ajira, kutowajibishwa kwa watendaji wasio waaminifu pamoja na kucheleweshwa kwa malipo ya wakandarasi.

“Natambua kuna ambao walikuwa na wakandarasi wao mkononi na kwa sababu hakupata basi fitina nyingi, anazuia miradi isifanyike kwa matakwa yake binafsi, hatutakwenda hivyo, ili tupate maendeleo ya haraka tunahitaji maamuzi ya haraka, “ amesema Rais Samia.

Samia amezisisitiza mamlaka zinazohusika kutofumbia macho mambo yatayokwamisha utekelezaji wa miradi kwa wakati ikiwemo kesi na mashauri ambayo hufunguliwa na wakandarasi wanaokosa tenda.


Soma zaidi


Ajira zitoke kwa wakati

Rais Samia  amekemea pia urasimu katika utoaji wa vibali vya ajira kwa wakandarasi kwa kuzitaka taasisi na mamlaka zinazohusika kutokuwa na mlolongo mrefu ambao unachelewesha utekelezaji wa mradi.

“Kama taasisi inataka wafanyakazi, mishahara ya kulipa wanayo, kwa mradi , kwa kazi fulani, wapewe ruhusa wafanye, ili miradi itekeleze kwa haraka, na kuzungushwa huku watu wanatafuta kupendeleana, tunadidimiza maendeleo,”  amesema Rais Samia kwa msisitizo.

Miongoni mwa miradi iliyotiwa saini leo ni pamoja na  mradi wa Ujazilizi 2B unaokusudia kupeleka umeme kwenye vitongoji 1,522, kupeleka umeme kwenye maeneo ya migodi, kilimo pamoja na vituo vya afya ambayo itagharimu Sh385 bilioni.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema kwa sasa umeme unaozalishwa bado hautoshi ingawa juhudi za Serikali kujinasua na jambo hilo zinaendelea.

“Tulipo kwenye umeme leo ndipo tulipokuwa kwenye barabara mwaka 1990, umeme hautoshi, miundombinu haitoshi lakini tunafarijika Rais umechukua maamuzi ya kishupavu kuwa shida ya umeme iishe, “ amesema Makamba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV