Njombe kinara maambukizi ya VVU Tanzania

November 25, 2026 6:06 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Mkoa wa Njombe umeendelea kushika nafasi ya kwanza nchini Tanzania kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), huku takwimu zikionyesha ongezeko la maambukizi katika mkoa huo ndani ya miaka nane.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania (THIS)  inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)mwaka 2016–2017 maambukizi ya VVU Njombe yalifikia asilimia 11.4.

Kasi ya maambukizi katika mkoa huo iliongezeka kwa asilimia 1.3 katika ripoti ya THIS ya 2022–2023 na kufikia asilimia 12.7 hali inayoashiria changamoto endelevu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kati ya idadi hiyo wanawake wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ni asilimia 16, mara mbili zaidi ya idadi ya wanaume iliyofika asilimia 8.6 .

Pamoja na idadi hiyo, watu wanaoishi na maambukizi  na kutambua hali zao wanawake ni asilimia 92.9, wanaume asilimia 92.0 ikiwa ni chini ya lengo la kitaifa la asilimia 95.

Mbali na Njombe mikoa mingine kinara kwa maambukizi ya VVU ni Iringa uliorekodi kasi ya maambukiizi ya kwa asilimia 11.1 katika ripoti ya mwaka 2022-2023 na Mbeya asilimia 9.

Kwa upande wa Iringa, kiwango cha maambukizi kimeonyesha kupungua kidogo kutoka asilimia 9.3 mwaka 2016–2017 hadi asilimia tisa mwaka 2022–2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Nov, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
DC Mpogolo: Marufuku kufanya biashara za mapishi, moto Buguruni Darajani.

DC Mpogolo: Marufuku kufanya biashara za mapishi, moto Buguruni Darajani.

Nukta TV

CHADEMA: Hakuna mazungumzo tutakayofanya hadi Tundu Lissu aachiwe huru

CHADEMA: Hakuna mazungumzo tutakayofanya hadi Tundu Lissu aachiwe huru

Nukta TV

Je, maridhiano ni sharti la lazima, kabla ya mchakato wa Katiba mpya?

Je, maridhiano ni sharti la lazima, kabla ya mchakato wa Katiba mpya?

Nukta TV