Euro, Pauni ya Uingereza zaimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania
- Dola ya Marekani haijaonyesha mabadiliko katika benki zote mbili.
Dar es Salaam. Viwango vya kubadilisha fedha za kigeni katika Benki ya CRDB na Benki ya NMB vimeongezeka kwa baadhi ya sarafu, ikiwemo Euro Pauni ya Uingereza kati ya Novemba 4 na 5, 2026.
Ulinganisho wa viwango vilivyochapishwa na benki hizo unaonyesha kuwa CRDB imeongeza bei ya kununua Euro kutoka Sh2,807.95 hadi Sh2,830.17, ikiwa ni ongezeko la Sh22.22 sawa na asilimia 0.79, huku bei ya kuuza Euro ikipanda kutoka Sh3,107.95 hadi Sh3,130.17 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.71.
Pauni ya Uingereza, CRDB imeongeza bei ya kununua kutoka Sh3,398.78 hadi Sh3,420.20, sawa na ongezeko la Sh21.42 huku bei ya kuuza ikiongezeka kwa kiasi hicho hicho, kutoka Sh3,698.78 hadi Sh3,720.20, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.58.
Kwa upande wa NMB, bei ya kununua Euro imepanda kutoka Sh2,799 hadi Sh2,802, ongezeko la Sh3, huku bei ya kuuza ikiongezeka kutoka Sh3,075 hadi Sh3,099, sawa ongezeko la Sh24.
Vilevile, benki hiyo imeongeza bei ya kununua Pauni kutoka Sh3,328 hadi Sh3,352, ikiwa ni ongezeko la Sh24 wakati bei ya kuuza ikipanda kutoka Sh3,682 hadi Sh3,706, sawa na ongezeko la Sh24.
Hata hivyo, viwango vya Dola ya Marekani havijabadilika katika benki zote mbili, huku CRDB ikiendelea kununua dola moja kwa Sh2,600 na kuuza kwa Sh2,680, wakati NMB ikiendelea kununua kwa Sh2,590 na kuuza kwa Sh2,670.
