Utamu wa rosti ya uyoga na viazi
- Uyoga una kati ya asilimia 20 hadi 35 ya protini ikiwa ni tofauti kabisa na mimea mingine suala linaloufanya uwe mbadala sahihi wa nyama.
Unapofikiria kupika rosti, huenda ukawaza nyama au kuku, lakini uyoga unaweza kuwa chaguo jingine la kutengeneza mlo wenye ladha unaoweza kuandaliwa kwa muda mfupi.
Pamoja na kuwa miongoni mwa mboga maarufu yenye ladha ya kipekee, tovuti ya Organicfacts inautaja uyoga kama ‘superfood’ kutokana na utajiri wake wa virutubisho muhimu na ikiwa na kiwango kidogo sana cha mafuta.
Tovuti hiyo inasema uyoga una kati ya asilimia 20 hadi 35 ya protini ikiwa ni tofauti kabisa na mimea mingine suala linaloufanya uwe mbadala sahihi wa nyama.
Mbali na protini uyoga pia una virutubisho vingine vingi kama Vitamaini B na D, nyuzi nyuzi na madini kama zinki na potashiam ambayo ni muhimu katika afya ya mwili wa mwanadamu.
Kwa wanaotaka kupunguza ulaji wa nyama uyoga unaweza kuwa mbadala, hivyo fuatana nasi katika makala hii tupike pamoja
Mahitaji
- Uyoga uliosafishwa na kukatwa vipande inaweza kuwa nusu kilo au kilo moja (inategemea na ukubwa wa familia au walaji) Maji kiasi

Hatua za kuandaa pishi lako la uyoga
Kabla hatujaanza mapishi ni ni muhimu kuhakikisha uyoga unaotumia ni ule unaoliwa na binadamu na sio aina nyingine ambazoo mara kadhaa huwa na sumu.
Ukisha upata uyoga utakaotumia hususan kama ni ule unaouzwa katika masoko makubwa au ‘supermarkets’ basi kazi ya kusafisha itakuwa ndogo kulinganisha na ule uliotoka porini moja kwa moja.
Ondoa sehemu zisizo hitajika kisha kata kata uyoga wako katika vipande vinavyolingana.
Baada ya hapo, andaa viungo na kuvikata kata kwa saizi upendayoo kisha washa jiko na ubandike sufuria yenye mafuta kiasi jikoni
Mafuta yakpata moto weka vitunguu maji jikoni na uvipike kwa dakika mbili hadi vitakapopata rangi ya kahawia
Ongeza kitunguu saumu killichotwangwa, nyanya na pilipili hoho kisha ukoroge kiasi na ufunike vilainike.
Nyanya ikiiva vizuri na kutengeneza mchuzi mzito kiasi ongeza chumvi na viungo vikavu unavyoependelea ikifuatiwa na uyoga uliokatwa vipande.
Kwa kawaida uyoga hutoa maji unapopikwa hivyo epuka kuongeza maji mengi mwanzoni, mpaka hapa unaweza ukaendelea kuacha jikoni kwa dakika saba hadi kumi hadi uyoga uive na kutoa mchuzi kiwango unachotaka.
Na mwisho kabisa unaruhusiwa kuonja ili kujua kiwango cha chumvi au viungo kulingana na ladha yako, ukiisha kujiridhisha basi unaipua chakula chako tayari kwaajili ya kuliwa.
Unaweza kutumia uyoga pamoja na wali, ugali chapati ama mkate, ukafurahia pamoja na familia, ndugu jamaa na marafiki.