Mrithi wa Ndejembi kujulikana Novemba 4, Chamwino

September 25, 2026 12:34 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Uchaguzi huo mdogo utafanyika Novemba 4, 2026, huku mchakato wa uteuzi wa wagombea ukitarajiwa kuanza Oktoba 7 kwa utoaji wa fomu za uteuzi.

Dar es Salaam. Mrithi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, Deogratius John Ndejembi, anatarajiwa kupatikana Novemba 4, 2026, baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo. 

Nafasi ya Ndejembi, aliyekuwa Mbunge wa Chamwino kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliachwa wazi kwa takriban siku 30 sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Agosti 26, 2026, kabla ya uteuzi huo kuthibitishwa na Bunge Agosti 28, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa INEC, Ramadhani Kailima, Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma.

Kailima amesema uchaguzi huo mdogo utafanyika Novemba 4, 2026, huku mchakato wa uteuzi wa wagombea ukitarajiwa kuanza Oktoba 7 kwa utoaji wa fomu za uteuzi.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fomu za uteuzi wa wagombea wa Ubunge Chamwino zitatolewa kuanzia Oktoba 7 hadi 13, 2026, huku siku ya uteuzi wa wagombea ikitarajiwa kuwa Oktoba 13.

Baada ya uteuzi, kampeni za uchaguzi zitaanza Oktoba 14 na kuendelea hadi Novemba 3, 2026, siku moja kabla ya wananchi wa Chamwino kwenda kupiga kura kumchagua mbunge atakayemrithi Ndejembi.

Ndejembi alichaguliwa kuwa Mbunge wa Chamwino kabla ya kuingia katika nafasi ya Waziri wa Nishati ambayo kwa sasa pia iko wazi huku Rais Samia akisubiriwa kufanya uteuzi wa kuziba nafasi hiyo.

INEC pia imetangaza kuwa Novemba 4, 2026 itatumika kufanya uchaguzi wa Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara, nafasi ambazo, kwa mujibu wa Tume, ziliachwa wazi kutokana na vifo vya madiwani wanane na kujiuzulu kwa madiwani watatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Nukta TV

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Nukta TV

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni  iwe nzuri

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni iwe nzuri

Nukta TV