‘Miss World’, AFCON zitakavyopaisha utamaduni wa Tanzania kimataifa

September 24, 2026 5:29 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Mbali na ngoma za asili, mashindano hayo pia yataipaisha lugha ya kiswahili kupitia wimbo maalum wa mashindano hayo kisha kutafsiriwa kiswahili.

Dar es Salaam. Hebu vuta picha, Mjerumani, Mwingereza au Mfaransa akicheza Mdundiko, ngoma ya asili ya Wazaramo,  mchiriku,  msondo ngoma au Bugobogobo, ngoma maarufu ya Wasukuma kutoka Kanda ya Ziwa.

Huenda picha hiyo ikawa miongoni mwa vivutio vya utamaduni wa Tanzania vitakavyoonekana na mamilioni ya watu duniani wakati wa mashindano ya 74 ya Mlimbwende wa Dunia (Miss World)

Tanzania imepata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwezi Mei 2027, baada ya kukabidhiwa rasmi bendera ya Mlimbwende wa Dunia na kusaini makubaliano ya uenyeji Aprili 20, 2026. 

Uenyeji huo utaifanya Tanzania kuwa nchi ya nne barani Afrika kuandaa mashindano hayo, baada ya Afrika Kusini, Seychelles na Nigeria, huku ikiwa ya kwanza Afrika Mashariki na Kati.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24, 2029 jijini Dar es Salaam amesema mashindano ya ‘Miss World’ (Ulimbwende) yatakayofanyika Tanzania mwaka 2027 yatakuwa na matukio makubwa manane, ikiwemo kuutangaza utamaduni wa Tanzania.

“Kila nchi itamleta ‘Miss’ “(Mlimbwende) wa nchi husika na huyo ‘Miss’ atapata fursa ya kuchagua kabila atakaloliwakilisha, atajifunza mambo muhimu yaliyopo kwenye kabila hilo na siku ya tukio atatakiwa kuwakilisha kabila hilo kwenye jukwaa la kidunia,” amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa, Tanzania ina zaidi ya makabila 120, hivyo mashindano hayo yatatoa fursa ya kutangaza, kukuza na kuendeleza tamaduni za makabila mbalimbali ya Tanzania.

https://www.instagram.com/p/DdrBCagz-zy/

Mbali na ngoma za asili, mashindano hayo pia yataipaisha lugha ya kiswahili kupitia wimbo maalum wa mashindano hayo kisha kutafsiriwa kiswahili na kuimbwa jukwaani na walimbwende hao.

 AFCON kuipeleka Tanzania kimataifa

Makonda amewaambia wanahabari kuwa utamaduni wa Tanzania utapaishwa pia katika anga za kitaiafa kupitia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa muziki, vyakula, mavazi, sanaa na lugha ya kiswahili.

Akieleza kuhusu maandalizi yanayotarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2026, Makonda ameeleza kuwa mpaka sasa miundombinu kuelekea AFCON 2027 yanaendelea vizuri, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo.

Kuwa mwenyeji wa mashindano hayo Tanzania imelipia takribani Dola za Marekani milioni 32 sawa Sh74 bilioni.

Hata hivyo, matukio ya mashindano hayo yatafanyika katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha.

Serikali imeeleza kuwa inalenga kutumia fursa hizo kuonesha Tanzania yenye utajiri wa tamaduni, huku ikihakikisha mila na desturi za jamii mbalimbali zinaendelezwa na kutambulika zaidi kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ukweli kuhusu Mama Fatma Karume, mwanamke aliyeshika kiganja cha historia ya Zanzibar

Ukweli kuhusu Mama Fatma Karume, mwanamke aliyeshika kiganja cha historia ya Zanzibar

Nukta TV

Tanzania yasisitiza amani na suluhu Mashariki ya Kati, kikao cha 81 cha UN

Tanzania yasisitiza amani na suluhu Mashariki ya Kati, kikao cha 81 cha UN

Nukta TV

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Nukta TV