Watoto Tanzania wanavyokabiliwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi

September 23, 2026 6:12 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ripoti ya UNICEF yaonyesha joto kali, moto, ukame na uchafuzi wa hewa ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili watoto

Dar es Salaam. Mabadiliko ya tabianchi yanazidi kushika kasi duniani, huku madhara yake yakijidhihirisha katika maisha ya kila siku kupitia ongezeko la joto, ukame, mafuriko na matukio mengine ya hali mbaya ya hewa.

Watoto ndio kundi linaloathirika zaidi na changamoto hizo kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) .

Ripoti ya Hatari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa Watoto 2026 iliyotolewa na shirika hilo hivi karibuni imebainisha kuwa takribani watoto bilioni 2 duniani wanakabiliwa na hatari mbili au zaidi za mabadiliko ya tabia ya nchi.

UNICEF inafafanua kuwa watoto bilioni 1.1 wengine wanakabiliwa na angalau hatari tatu na watoto bilioni 2.3 wanaishi katika maeneo yanayokabiliwa na angalau hatari moja ya mabadiliko ya tabianchi.

Tanzania Hatarini

Ripoti hiyo imefafanua zaidi kuwa Tanzania inaingia katika orodha ya nchi ambazo watoto wako hatarini kukumbanana na athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uchafuzi wa hewa, mawimbi ya joto, moto, ukame, mafuriko na dhoruba za mchanga na vumbi.

UNICEF imebainisha kuwa Tanzania imepata alama 4.62 kati ya 10 katika kipimo kinachotathimini kiwango cha watoto wanaokabiliwa na hatari nyingi za tabianchi.

Alama hiyo inamaanisha kuwa watoto nchini Tanzania wanakabiliwa na kiwango cha kati cha hatari za mabadiliko ya tabianchi.

Katika matokeo hayo ya athari za tabianchi kwa watoto Tanzania imepata alama 4.64 kwa mawimbi ya joto, (alama 4.56 katika matukio ya moto), (alama 3.20 kwa ukame), (alama 1.91 kwa mafuriko ya mito), (alama1.20 kwa mafuriko), (1.02 kwa dhoruba za kitropiki) na alama 1.75 kwa dhoruba za mchanga na vumbi.

Ili kukabiliana na matatizo ya tabianchi yanayowakumba watoto, ripoti inapendekeza kuimarisha huduma muhimu kama afya, lishe, maji safi, elimu na ulinzi wa watoto. 

Pia, Serikali zinapaswa kuanzisha mifumo ya tahadhari za mapema, kujenga shule na vituo vya afya vinavyostahimili majanga ya tabianchi, pamoja na kutoa msaada wa dharura kwa watoto na familia zilizoathirika.

Aidha, ripoti inasisitiza umuhimu wa kuwashirikisha watoto na vijana katika maamuzi yanayohusu tabianchi, kuongeza elimu ya mazingira na kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
23 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Nukta TV

Othman Masoud: Serikali ya Umoja wa Kitaifa si mwisho wa safari ya watu wa Zanzibar

Othman Masoud: Serikali ya Umoja wa Kitaifa si mwisho wa safari ya watu wa Zanzibar

Nukta TV

OTHMAN MASOUD alivyoapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

OTHMAN MASOUD alivyoapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

Nukta TV