NMB, CRDB zatoboa orodha ya benki 500 Forbes

September 16, 2026 4:19 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni katika orodha ya benki zinazofanya vizuri zaidi duniani kwa mwaka 2026.
  • Katika kundi la Tier 6, linalojumuisha benki zenye mali kati ya Dola bilioni 3 na 10 za Marekani, NMB imechukua nafasi ya tisa, huku CRDB ikiwa ya 41. 

Dar es Salaam. Sekta ya fedha nchini Tanzania imeingia katika sura mpya baada ya benki za CRDB na NMB, kuingia kwenye orodha ya benki 500 zinazofanya vizuri zaidi duniani kwa mwaka 2026 hatua inayoweka taasisi hizo kwenye jukwaa la kimataifa la benki zilizopimwa kwa utendaji wao wa kifedha.

Benki hizo zimepenya katika orodha hiyo iliyozingatia uwezo wa benki kuzalisha faida, ukuaji, ubora wa mapato, uimara wa mtaji na vyanzo vya fedha, pamoja na ubora na ufanisi wa mali kutoka katika mataifa 89 duniani kote. 

Jarida la Forbes la nchini Marekani kwa kushirikiana na kampuni ya utafiti ya Statista, limeziweka benki hizo katika kundi la sita (Tier 6) linalojumuisha linalojumuisha benki zenye mali kati ya Dola za Marekani bilioni 3 hadi 10.

Katika orodha hiyo, NMB imechukua nafasi ya tisa kizichakaza benki nyingine 41 kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo mataifa ya Falme za Kiarabu (UAE) na Marekani, huku CRDB ikishikilia nafasi ya 41.

Kwa upande wa faida, kwa pamoja benki hizo zimepewa uzito wa asilimia 30, asilimia 25 kwa uimara wa mtaji na vyanzo vya fedha, asilimia 25 kwa ubora na ufanisi wa mali huku ubora wa ukuaji na ubora wa mapato ukipewa asilimia 20.

Hii ina maana kwamba NMB na CRDB, ambazo ni miongoni mwa benki kubwa za biashara nchini, zimeendelea kuimarika katika utendaji wa kifedha, jambo linaloonyesha nafasi yao muhimu katika sekta ya benki, biashara na uchumi wa Tanzania. 

NMB, CRDB zarekodi ukuaji wa mapato na faida 

Utendaji huo wa kimataifa unaenda sambamba na matokeo ya kifedha ya benki hizo nchini, ambazo zote zimeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). 

Kwa mwaka wa fedha ulioishia Desemba 2025, mapato ya uendeshaji ya CRDB yalifikia Sh1.884 trilioni, sawa na ongezeko la asilimia 24.1, huku faida kabla ya kodi ikipanda kwa asilimia 32.3 hadi Sh1.031 trilioni na faida baada ya kodi ikiongezeka kwa asilimia 32.1 hadi Sh728.6 bilioni. 

Kwa upande wa NMB, ambayo hivi karibuni ilipata fedha kupitia bondi ya Dola za Marekani milioni 100 ya IFC iliyoorodheshwa katika Soko la Hisa la London, mapato yake yalifikia Sh1.825 trilioni mwaka 2025, yakiongezeka kwa asilimia 13.3, huku faida kabla ya kodi ikifika Sh1.067 trilioni na faida baada ya kodi Sh760 bilioni, sawa na ongezeko la asilimia 15 na 17 mtawalia.

Bondi hiyo, yenye thamani ya takriban Sh262.5 bilioni, inalenga kuwezesha NMB kuongeza ufadhili kwa biashara, hususan sekta ya biashara ndogo na za kati (SMEs)

Hata hivyo, NMB na CRDB si benki pekee kutoka Afrika Mashariki zilizofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo.

Kutoka Kenya, KCB Group, Equity Group, Co-operative Bank na Stanbic Holdings zimeingia kwenye orodha hiyo, huku RawBank ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa miongoni mwa benki nyingine za ukanda huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Sio nyama na matunda tu, Wahadzabe sasa wanakula ugali

Sio nyama na matunda tu, Wahadzabe sasa wanakula ugali

Nukta TV

Haya ndio mambo waajiri huangalia kipindi cha probation

Haya ndio mambo waajiri huangalia kipindi cha probation

Nukta TV

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nukta TV