World Bank Group yamteua Mary-Jean Moyo kuongoza IFC mataifa sita

September 16, 2026 3:39 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Zambia na Zimbabwe.

Dar es Salaam. Benki ya Dunia (World Bank Group) imemteua raia wa Zimbabwe Mary-Jean Moyo kuwa Mkurugenzi wa Divisheni wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) anayesimamia shughuli za shirika hilo Tanzania na nchi nyingine tano za Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na World Bank, Moyo ameanza rasmi majukumu hayo Septemba 1, 2026, ambapo atakuwa akisimamia shughuli za IFC nchini Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Zambia na Zimbabwe.

IFC ni taasisi ya Benki ya Dunia inayolenga zaidi maendeleo ya sekta binafsi katika masoko yanayoibukia, ikifanya kazi katika zaidi ya nchi 100 kwa kutumia mtaji, utaalamu na ushawishi wake kuchochea masoko na fursa za biashara.

Kwa uteuzi huo, Moyo anawajibika kushughulikia uwekezaji wa sekta binafsi, kusaidia ukuaji wa biashara na kuchochea uanzishwaji wa ajira zaidi na zenye tija katika nchi hizo sita.

Kwa mujibu wa IFC, uteuzi huo unaenda sambamba na msisitizo wa Benki ya Dunia wa kufanya kazi kwa mtazamo wa taasisi moja katika kusaidia vipaumbele vya nchi wanachama, kwa kuunganisha sera na uwekezaji wa sekta ya umma na utaalamu, fedha na huduma za ushauri za IFC kwa sekta binafsi.

Dsm kuwa kitovu cha uratibu shughuli za IFC

Uteuzi wa Moyo unakuja wakati IFC ikiendelea kuongeza nafasi yake katika kufadhili sekta binafsi katika masoko yanayoendelea.

Katika mwaka wa fedha 2026, IFC ilitoa ahadi za uwekezaji zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 71.7 kwa kampuni binafsi na taasisi za fedha katika nchi zinazoendelea.

Kwa mujibu wa World Bank, katika utekelezaji wa majukumu yake, Moyo atakuwa akifanya shughuli zake kutokea jijini Dar es Salaam akisimamia ushirikiano wa IFC katika mataifa yaliyochini ya jukumu lake.

Nafasi hiyo inaifanya Dar es Salaam kuwa kitovu cha uratibu wa shughuli za IFC, hususan katika juhudi za kuongeza mtaji binafsi, kuendeleza biashara na kusaidia ajira.

Uzoefu katika sekta ya fedha 

Moyo ameingia katika nafasi hiyo akiwa na uzoefu katika fedha za maendeleo, uwekezaji wa sekta binafsi, benki za biashara na uongozi wa taasisi, akiwa amefanya kazi katika maeneo mbalimbali barani Afrika, Amerika Kusini na Karibiani pamoja na Mashariki ya Kati.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Wafanyakazi (Chief of Staff) wa Mkurugenzi Mtendaji wa IFC.

Awali, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kanda wa Viwanda katika sekta za uzalishaji, kilimo na huduma kwa Mashariki ya Kati na Afrika, ambako alishiriki katika kusimamia utekelezaji wa malengo ya biashara na athari za maendeleo, pamoja na kuongeza uwekezaji katika nchi zinazostahili kupata msaada kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) na maeneo yaliyoathiriwa na migogoro.

Pia aliwahi kuwa mkuu wa kanda wa sekta hizo hizo kwa IFC Amerika Kusini na Karibiani, akisimamia ukuzaji wa biashara, utekelezaji wa uwekezaji na usimamizi wa miradi iliyokuwa tayari katika mfuko wa uwekezaji.

Akizungumza kuhusu jukumu lake jipya, Moyo amesema kuna fursa kubwa ya kuongeza uwekezaji binafsi, kuimarisha biashara na kuunda ajira zenye ubora Afrika Mashariki .

“Nimefurahi kurejea katika ukanda huu na kuwa Dar es Salaam tunapoimarisha ushirikiano wetu na Serikali, sekta binafsi na washirika wa maendeleo.

Kwa pamoja, tunaweza kusaidia kuvutia mitaji, kuunga mkono ujasiriamali, uvumbuzi na kuchochea ukuaji jumuishi na endelevu unaoleta manufaa yanayoonekana kwa watu katika kanda nzima,” amesema Moyo.

Uzoefu kabla ya IFC

Kabla ya kujiunga na IFC, Moyo alifanya kazi katika benki za biashara nchini Zimbabwe, Benki Kuu ya Botswana pamoja na mifuko ya uwekezaji binafsi inayofanya kazi katika nchi mbalimbali za Afrika.

Katika sekta ya uwekezaji binafsi, aliwahi kuwa Makamu wa Rais anayesimamia taasisi za fedha.

Moyo ana shahada ya uzamili ya Banking and Finance kutoka University of Wales na shahada ya kwanza ya Economic History kutoka University of Zimbabwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Sio nyama na matunda tu, Wahadzabe sasa wanakula ugali

Sio nyama na matunda tu, Wahadzabe sasa wanakula ugali

Nukta TV

Haya ndio mambo waajiri huangalia kipindi cha probation

Haya ndio mambo waajiri huangalia kipindi cha probation

Nukta TV

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nukta TV