TASAC yasitisha utoaji leseni za bandari kavu

August 31, 2026 7:00 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa lengo la kupunguza usumbufu unaowakabili wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo.

Dar es Salaam. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesitisha kwa muda utoaji wa leseni mpya za uendeshaji wa bandari kavu (ICD), likisema hatua hiyo inalenga kudhibiti uanzishwaji wa vituo hivyo katika maeneo yasiyokidhi vigezo na kupunguza usumbufu unaowakabili wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo.

Uamuzi huo unakuja wakati ambapo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi, hasa jijini Dar es Salaam, kuhusu kuongezeka kwa bandari kavu katika maeneo ya makazi na athari zake, ikiwemo ongezeko la malori, msongamano wa magari, kelele na changamoto nyingine za kimazingira na kiusalama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Malick Salum, amesema shirika hilo limeamua kusitisha utoaji wa leseni mpya baada ya kubaini umuhimu wa kufanya tathmini ya kina zaidi kabla ya kuruhusu uanzishwaji wa bandari kavu.

Amesema awali mchakato wa kupata vibali ulihusisha taasisi mbalimbali, ikiwemo mamlaka za mipango miji, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kabla ya nyaraka hizo kuwasilishwa TASAC kwa ajili ya mchakato wa utoaji leseni.

Kwa mujibu wa Salum, mfumo huo ulifanya TASAC kutokuwa na nafasi ya kutosha kufanya upembuzi mpana wa eneo linalopendekezwa kuanzishwa bandari kavu, hususan kwa kuangalia athari zake kwa makazi ya wananchi na mtiririko wa magari.

“Mtu asiendeleze eneo lolote bila kupata kibali chetu kama taasisi ili kuona kama kunafaa, lakini baada ya kuona kelele zaidi tukaamua kusimamisha zoezi la utoaji leseni za bandari kavu. Kwa hiyo sasa hivi hatutoi leseni za bandari kavu,” amesema Salum. 

Lakini ICD bado ni muhimu

Pamoja na kusitisha utoaji wa leseni mpya, TASAC inasisitiza kuwa uwepo wa bandari kavu ni sehemu muhimu ya mnyororo wa usafirishaji wa mizigo na hauwezi kuondolewa kwa sababu tu ya changamoto zinazojitokeza katika baadhi ya maeneo.

Mkurugenzi Udhibiti Uchumi wa TASAC, Nahson Sigalla, amesema mahitaji ya bandari kavu yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uwezo mdogo wa eneo la Bandari ya Dar es Salaam kuhifadhi makontena kwa wakati mmoja, ikilinganishwa na kiasi cha mizigo kinachopitia bandarini.

Sigalla amesema Bandari ya Dar es Salaam inapokea zaidi ya makontena 110,000 kwa mwezi, wakati uwezo wa eneo la ndani ya bandari kuhifadhi makontena ni takribani 27,000 kwa wakati mmoja.

Takwimu hizo zinaonyesha kwa nini huduma za kuhifadhi na kushughulikia mizigo haziwezi kufanyika zote ndani ya bandari yenyewe, hivyo kuifanya miundombinu ya bandari kavu kuwa sehemu muhimu ya kupunguza msongamano bandarini.

Kwa wastani, zaidi ya makontena 110,000 kwa mwezi ni sawa na zaidi ya makontena milioni 1.3 kwa mwaka, jambo linaloweka shinikizo kubwa kwa miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam na mfumo mzima wa usafirishaji.

“Kama makontena mengi [yatajaa bandarini] bandari itasimama, na ikisimama maana yake gharama zitaongezeka kwenye mnyororo mzima,” amesema Sigalla.

Kwa TASAC, hoja si kuondoa bandari kavu, bali kuhakikisha vituo hivyo vinajengwa na kuendeshwa katika maeneo yanayofaa na kwa kuzingatia mahitaji ya miundombinu, usalama, mazingira na wananchi.

Suluhisho litafutwe, si kusimamisha sekta

Mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji wa Bandari Kavu za Forodha Tanzania (CIDAT), Meleck Shange, amesema waendeshaji wa bandari kavu na mamlaka wanaendelea kushirikiana kutafuta namna ya kushughulikia changamoto zinazotokana na uwepo wa vituo hivyo katika maeneo mbalimbali.

CIDAT inawakilisha wadau wanaojihusisha na vituo vya mizigo ya makontena (CFS), bandari kavu (ICDs), vituo vya kuhifadhia makontena matupu pamoja na magari yanayosafirisha mizigo kwenda na kutoka katika bandari kavu nchini. 

Shange amesema sekta hiyo ina umuhimu mkubwa katika kusaidia kupunguza shinikizo linalowekwa na ongezeko la mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, hivyo suluhisho linapaswa kulenga kuboresha maeneo na namna vituo hivyo vinavyoendesha shughuli zao badala ya kuathiri mnyororo mzima wa usafirishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
31 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Matarajio ya wachambuzi wa siasa na uchumi kwa Ndejembi

Matarajio ya wachambuzi wa siasa na uchumi kwa Ndejembi

Nukta TV

Maagizo mazito ya Rais Samia kwa Ndejembi

Maagizo mazito ya Rais Samia kwa Ndejembi

Nukta TV

Ndejembi alivyoapa mbele ya Rais Samia kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Ndejembi alivyoapa mbele ya Rais Samia kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Nukta TV