TAFFA kutumia mfumo wa kielektroniki kurahisisha huduma za forodha

July 30, 2026 11:26 am · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link

  • Ni kuanzia Agosti 1, 2026, utatumika kushughulikia mizigo inayoingizwa na kutoka kupitia bandarini na mipakani.

Dar es Salaam. Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kimetangaza kutumia mfumo wa kielekroniki utakaorahisisha shughuli za uingizaji na usafirishaji wa bidhaa, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi, uwazi na kasi ya utoaji wa huduma katika sekta ya biashara na usafirishaji nchini.

Mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia Agosti 1, 2026, ukiwa umeunganishwa na mfumo wa Tanzania Electronic Single Window (TANESW), unaoratibu huduma za taasisi mbalimbali zinazohusika na biashara ya kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAFFA  mfumo huo utatumika katika shughuli za uingizwaji wa bidhaa nchini, usafirishaji wa bidhaa kwenda nje na mizigo ya transist inayosafirishwa kwenda nchi jirani kupitia Tanzania.

Hata hivyo, chama hicho kimeeleza kuwa bidhaa na huduma zilizoondolewa kwenye utaratibu huo kwa mujibu wa Notisi ya Serikali (GN) Na. 83 ya mwaka 2026 hazitahusika na matumizi ya mfumo.

Kabla ya kuanza kutumika kwa wadau wote, TAFFA imesema utekelezaji utaanza kwa majaribio kwa kushirikiana na baadhi ya kampuni za uwakala wa forodha ili kuhakikisha mfumo unafanya kazi kwa ufanisi na kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji.

Aidha, chama hicho kimewataka wanachama wake pamoja na wadau wengine wa biashara kuanza kujiandaa kwa matumizi ya mfumo huo kwa kufuatilia taarifa rasmi zitakazotolewa kuhusu usajili, mafunzo na taratibu za matumizi.

Suluhu ya changamoto za biashara

Utumiaji wa mifumo ya kielektroniki katika baadhi ya taasisi za Serikali unakuja wakati ambapo kwa muda mrefu wananchi na wafanyabiashara wamekuwa wakikumbana na changamoto zinazotokana na mifumo ya taasisi za umma kutosomana. 

Hali hiyo imekuwa ikisababisha urudufu wa taarifa, ucheleweshaji wa toaji wa huduma, gharama za ziada za kufanya biashara, pamoja na kupoteza muda kwa wananchi na wawekezaji waliolazimikau kuwasilisha taarifa zilezile katika taasisi tofauti. 

Huenda sasa matumizi ya mifumo ya kidijitali inayosomana yakawa suluhisho la changamoto zilizodumu kwa muda mrefu kwa kurahisisha uratibu wa huduma za Serikali, kupunguza urasimu na muda wa utoaji huduma, kuimarisha uwazi, kuboresha mazingira ya biashara, pamoja na kurahisisha uingizaji na usafirishaji wa mizigo, hivyo kuongeza ushindani wa Tanzania kama kitovu cha biashara na usafirishaji katika Afrika Mashariki. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
30 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Vodacom Tanzania yapendekeza gawio la Sh23.91 kwa hisa 2026

Vodacom Tanzania yapendekeza gawio la Sh23.91 kwa hisa 2026

Nukta TV

Fursa kwa wakulima, uhitaji mazao ya chakula ukiongezeka Kenya, Uganda

Fursa kwa wakulima, uhitaji mazao ya chakula ukiongezeka Kenya, Uganda

Nukta TV

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Nukta TV