TRA yavuka lengo ikikusanya Sh37.96 trilioni 2025/26

July 4, 2026 3:18 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni sawa na asilimia 105.24 ya lengo kulinganisha na lengo la Sh36.07 lililokusudiwa kukusanywa.
  • Kiwango kilichokusanywa mwaka 2025/26 ni cha juu kuwahi kurekodiwa. 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya mapato ya Sh37.96 trilioni katika mwaka wa fedha 2025/26 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa na taasisi hiyo tangu ianzishwe. 

Mapato hayo yaliyokusanywa kati ya Julai 2025 na Juni 2026, yamevuka lengo kwa zaidi Sh1.89 trilioni au asilimia 105 ya lengo la kukusanya Sh36.07 trilioni. 

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda Julai 3, 2026 inabainisha kuwa makusanyo hayo yameongezeka kwa takriban asilimia 18 ikilinganishwa na Sh32.27 trilioni zilizokusanywa mwaka 2024/25. 

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa TRA kuvuka lengo la makusanyo tangu walipofanya hivyo katika mwaka wa fedha uliotangulia ambao walikusanya asilimia 104 ya lengo.

“TRA imefanikiwa kufikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa miezi 24 mfululizo kuanzia Julai 2024 mpaka Juni 2026, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya utendaji wa Mamlaka,” imeeleza taarifa hiyo ya TRA.

Kuvuka lengo kwa TRA kwa miaka miwili mfululizo kunaipa Serikali fursa ya kugharamia miradi ya maendeleo na huduma za kijamii kupitia mapato ya ndani hasa katika kipindi ambacho misaada imekuwa ikipungua mwaka hadi hadi kutokana Marekani na mataifa ya Ulaya kubadili sera za misaada. 

Kwa mwaka 2025 mwezi Desemba ndio mwezi ulioongoza kwa makusanyo ya juu zaidi ndani ya mwezi mmoja ukikusanya Sh4.13 trilioni huku wastani wa makusanyo ya mwezi ukipanda hadi Sh3.16 trilioni kutoka Sh2.69 trilioni mwaka uliotangulia.

Uchambuzi uliofanywa na Nukta Habari umebaini kuwa miezi ya Januari na Aprili 2026 ilirekodi ukuaji mkubwa zaidi kwa mwaka hadi mwaka, ambapo Januari mapato yaliongezeka kwa takriban asilimia 25.91 huku Aprili ikirekodi ongezeko la asilimia 26.21. 

Kwa mujibu wa TRA mafanikio haya yamechagizwa na upanuzi wa mifumo ya kidijitali, hususan kuanza rasmi kwa mfumo mpya wa usimamizi wa kodi za ndani wa IDRAS uliounganisha taasisi 82 za umma na binafsi. 

Ndani ya mwaka mmoja TRA imesajili walipakodi wapya 1,400,810 na kufanya idadi ya waliosajiliwa kufikia 8,564,172 hadi Juni 30, 2026, sawa na ukuaji wa takriban asilimia 20 ikilinganishwa na walipakodi 7,163,362 waliokuwapo Juni 2025.  

Utendaji huo unakuja wakati zaidi Serikali inaanza utekelezaji rasmi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaolenga kuongeza uchumi wa Tanzania mara 10 zaidi ya sasa kufikia uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja au zaidi Sh2,600 trilioni ifikapo mwaka 2050.

Mamlaka hiyo pia inasema kampeni za elimu ya kodi, utatuzi wa migogoro nje ya mahakama na ufuatiliaji wa karibu wa mizigo mipakani vimechangia kuongeza mapato kwa kiasi kikubwa hadi kufikia kuvuka lengo.

Kupitia dawati la kuwezesha biashara, changamoto 68,650 za wafanyabiashara zilitatuliwa hadi Mei 2026, hatua iliyosaidia kulinda kodi ya Sh508.89 bilioni ambayo ingepotea kama biashara hizo zingekwama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV