Mwenendo wa deni la Taifa kwa miaka 10

June 13, 2026 2:55 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko hilo limetokana na mikopo mipya na inayoendelea kutolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Dar es Salaam. Miongoni mwa mada zinazotawala mijadala katika mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali nchini Tanzania ndani ya siku tatu zilizopita, ni suala la deni la taifa.

Mjadala huo umeibuka baada ya Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Omar, kueleza kuwa deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 8.97 na kufikia Sh114.34 trilioni kufikia Machi 2026 kutoka Sh104.93 trilioni katika kipindi kama hicho mwaka 2025

Balozi Omar aliyekuwa akiwasilisha bajeti ya Serikali bungeni Dodoma Juni 11,2026b amesema deni hilo linaweza kuongezeka ikitarajia kukopa Sh15.54 trilioni katika mwaka wa fedha 2026/27.

Ongezeko hilo limetokana na mikopo mipya na inayoendelea kutolewa kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo nchini.

Kabla ya kuendelea kuchambua mwenendo wa deni hilo, ni muhimu kujiuliza; Tanzania ilianza lini kukopa? 

Kwa mujibu wa kumbukumbu mbalimbali za kiuchumi, Tanzania ilianza rasmi kukopa kutoka kwa mataifa na taasisi za kifedha za kimataifa miaka michache baada ya kupata uhuru mwaka 1961. 

Kiwango cha ukopaji kiliongezeka zaidi kuanzia miaka ya 1970 kufuatia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, changamoto za kiuchumi zilizotokana na vita vya Kagera, kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kupungua kwa mapato ya mauzo ya mazao ya nje.

Nukta tv imefanya uchambuzi wa mwenendo wa bajeti hiyo ndani ya miaka 10 iliyopita na kubaini kuwa deni la taifa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka ikisaidia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kisasa (SGR), mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), upanuzi wa viwanja vya ndege, barabara na sekta nyingine za maendeleo.

Mthalan, Mwaka 2016, deni la taifa lilikuwa takribani Sh38.07 trilioni Mwaka 2017 liliongezeka na kufikia Sh42.88 trilioni, huku mwaka 2018 likifikia Sh50.77 trilioni ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 33.36 kwa miaka mitatu

Mwaka 2019 deni hilo lilikuwa Sh50.77 trilioni kabla ya kufikia Sh55 trilioni, mwaka 2020. 

Deni hilo liliendelea kupaa hadi Sh59.85 trilioni mwaka 2021 na mwaka uliofuata yaani mwaka 2022 likafikia Sh69.26 trilioni.

Mwaka 2023 likafikia Sh77.01 trilioni na mwaka 2024 deni lilikuwa Sh97.35 trilioni sawa na ongezeko la asilimia 26.41 ndani ya mwaka mmoja. 

Hata hivyo, Ongezeko hilo bado liliendelea mpaka mwaka 2025 ambapo aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba alisema kuwa hadi Aprili 2025, deni la Serikali lilikuwa Sh107.70 trilioni na kati ya kiasi hicho, deni la nje ni Sh72.94 trilioni na deni la ndani ni Sh34.76 trilioni.

“Hadi Aprili 2025, jumla ya deni la serikali lilikuwa Sh107.70 trilioni. Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa trilioni 72.94.Tathmini iliyofanyika mwaka 2024 inaonyesha kuwa  katika vipindi vya muda mfupi, kati, na mrefu,” alieleza.

Aidha, mpaka kuisha kwa mwaka huo jumla ya deni ilikuwa Sh110.25 trilioni likiongezeka hadi kufika Sh114.34 trilioni Machi mwaka huu licha ya Serikali kusisitiza kuwa deni hilo bado ni himilivu na linaendelea kubaki ndani ya viwango vinavyokubalika kimataifa. 

Kwa ujumla, katika kipindi cha miaka kumi kuanzia 2016 hadi 2026, deni la taifa limeongezeka kwa takribani asilimia 200.34, kutoka Sh trilioni 38.07 hadi Sh114.34 trilioni .

Hii ina maana kwamba deni la taifa mwaka 2026 ni karibu mara tatu ya kiwango kilichokuwepo mwaka 2016.

Lakini safari ya ukopaji bado haijaisha. Katika mwaka wa fedha 2026/27, Serikali imepanga kukopa jumla ya Sh15.54 trilioni.

Wachambuzi watia neno

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya fedha, Paul Chengula kutoka Dar es Salaam, nchi kukopa si tatizo, muhimu ni kuhakikisha fedha zinazokopwa zinaelekezwa kwenye miradi yenye tija inayozalisha mapato na kuongeza uwezo wa nchi kulipa madeni yake siku zijazo.

“Nchi kukopa sio dhambi. Inategemeana sasa na hiyo nchi inakopa lakini hiyo mikopo inayopata inaitumia katika mambo gani? Kama endapo inaitumia katika maswala ya ‘development activities’ (kazi za maendeleo) ambazo baadaye zinaenda zinazalisha…

… Hilo ni deni ambalo ni tunasema ni mikopo vizuri lakini kama endapo nchi inakopa lakini inaenda kutumia ile mikopo kwa ajili ya kuspend kwenye matumizi ya kawaida ambayo hayazalishi tunasema hiyo mikopo inakuwa sio mizuri sana,” amesema Chengula 

Hata hivyo, anashauri Tanzania ianze kuongeza mapato yake ya ndani kupitia kodi na vyanzo vingine vya mapato ili kupunguza utegemezi wa mikopo ya nje.

“Tunachotakiwa tufanye tupunguze hiyo mikopo ya nje. Tuanze sasa kutumia mapato yetu ya ndani mapato upande wa kodi na kadhalika. Tuongeze vyanzo vya kodi ili tupunguze sasa kuegemea zaidi kwenye mikopo hiyo,” ameongeza mchambuzi huyo.

Je, ongezeko la deni la taifa ni mzigo kwa kizazi cha sasa na kijacho, au ni uwekezaji unaolenga kuharakisha maendeleo ya uchumi wa Tanzania? 

Hilo ndilo swali linaloendelea kugawanya maoni ya wananchi, wachumi na wanasiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV