Rais Samia aagiza kuundwa kwa kikosi kazi cha nishati safi ya kupikia 

November 2, 2022 12:06 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kitatoa mwelekeo wa kitaifa juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
  • Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha inaokoa maisha ya Watanzania wanaofariki kila mwaka  kutokana na kuvuta moshi wa kuni.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu ameagiza kuundwa kwa kikosi kazi kitakachotoa mwelekeo wa kitaifa juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kikosi kazi hicho kitakachohusisha sekta binafsi na wadau wa maendeleo kitakuwa na kazi ya kuchambua sera za Serikali na mapendekezo ya wadau mbalimbali kikiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa huku uratibu utafanyika chini ya Wizara ya Nishati.

“Kwenye hili Serikali peke yetu hatuwezi tunapaswa kwenda sambamba na sekta binafsi, nashukuru baadhi yao wameanza kujitokeza,” amesema  Rais Samia jana Novemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mjadala wa kitaifa kuhusu nishati safi ya kupikia.

Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha inaokoa maisha ya Watanzania wanaofariki kila mwaka  kutokana na kuvuta moshi wa kuni.

Inakadiriwa kuwa watu 33,000 nchini Tanzania wanafariki dunia kila mwaka kutokana na kuvuta sumu za moshi unaotoka kwenye kuni na mkaa wakati wa kupika. 

Mbali na athari za kiafya ambazo zinachangia uwepo wa zaidi ya theluthi mbili ama asilimia 70 za magonjwa ya upumuaji, matumizi ya nishati zisizo safi yanachangia ongezeko la hewa ya ukaa inayochafua mazingira na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Amesema kikosi kazi hicho kitakuja na mpango mkakati ambao utaiongoza Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutafuta suluhu ya nishati safi na endelevu ya kupikia.

Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati, kaya zinazopikia kwa kutumia mitungi ya gesi ni asilimia 5, umeme (asilimia 3) na nishati nyingine safi asilimia 2.2.

“Hii inaonyesha bado kuna kazi ya kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo safi na salama. Tunapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kisera na kibajeti pamoja na kuweka mazingira wezeshi katika kutatua changamoto za upatikanaji wa nishati safi,” amesisitiza Rais. 

Mpango wa Serikali ni kuhakikisha mpaka mwaka 2032 inafikia asilimia 80 hadi 90 ya Watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV