Mapishi ya chai ya nazi za Pangani

January 6, 2024 11:40 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Utahitaji tui la nazi zito kikombe 1 na robo na viungo vingine.
  • Unaweza kusindikiza chai hii na kitafunwa chochote.

Najua unazifahamu sifa za jiji la Tanga, husuan ile ya uwepo wa nazi nyingi zinazotumika kuandaa mapishi mbalimbali.

Kutokana na kuenea kwa sifa hizo nikadhamiria kwenda kumtembelea rafiki yangu anayeishi Pangani Jijini Tanga, kichwani nikawaza kkumuandalia  chai ya nazi ambayo si maarufu sana katika maeneo haya.

Lengo la kuvutiwa na aina hiyo ya kifungua kinywa ni kuwadhihirishia wakazi wa jiji hilo kuwa hata watu wa mikoa mingine tupo vizuri kwenye mapishi.

Baada ya kuandaa chai hiyo, rafiki yangu aliipenda sana na ‘kunimwagia maua yangu’ nikasema acha nije niwafundishe wasomaji wa jiko point wapate kuongeza ujuzi na  maujanja jikoni.

Utamu wa chai ya nazi huchangiwa zaidi yaaina ya viungo unavyoweka, chagua vile ambavyo wewe au familia yako inavipenda zaidi.Picha|

Mahitaji

Kwanza ukitaka kupika chai hii utahitaji tui la nazi zito kikombe 1 na robo, hapa unaweza kutumia nazi freshi au ya pakiti inayopatikana kirahisi madukani.

Utahitaji maji safi kikombe kimoja na nusu ili kuongeza wingi wa chai yako, majani ya chai kijiko kimoja cha chai, sukari kiasi kulingana mahitaji yako, iriki, mdalasini, majani ya oregano, mints (nanaa) pamoja na karafuu kama unapendelea.

Hakikisha nazi unazozitumia zimekomaa ili kuweza kupata tui zito zaidi.Picha|Neema Herbalist.

Karibu jikoni tuandae pamoja

Anza mapishii yako kwa kusafisha sufuria utakayopikia, washa jiko, na ubandike sufuria na umimine maji pamoja na tui lanazi uliloliandaa.

 Hatua inayofuata ni kuweka viungo vyote vinavyohitajika katika pishi hili. Hakikisha umevitwanga na kuchekecha vizuri kisha uache ichemke.

Kama ilivyo kwa mapishi mengine yanayotumia nazi, ni mwiko kufunika chai yako kabla haijachemka ili kuzuia tui kukatika.

Mchanganyiko ukianza kuchemka  punguza moto kiasi kisha acha ichemke taratibu ili iingie viungo kwa muda wa dakika sita.

Ongeza tena tena moto kama awali na acha ichemkie kwa muda wa dakika 10 kisha epua,chuja na itakuwa tayari kwa kunywa.

Chai hii ni tamu sana na unaweza kuinywa kwa vitafunwa mbalimbali kama vile skonzi, mandazi ya kuoka, chapati za amira, na aina nyingine nyingi.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV