Fahamu umuhimu wa kutumia mafuta ya nazi katika mapishi

August 7, 2025 12:21 pm · Zakia Mrisho
Share
Tweet
Copy Link
  • Husaidia kuimarisha afya ya moyo na mmengenyo wa chakula.
  • Husaidia kupunguza uzito wa mwili.

Mafuta ya nazi ni miongoni mwa mafuta ya asili yanayotumika sana katika shughuli mbalimbali ikiwemo urembo wa ngozi na nywele.

Umaarufu wa mafuta haya ya asili yanayotokana na nazi ambazo hupitia michakato tofauti hadi kutumiwa kwa ajili ya urembo au maandalizi ya chakula.

Ndio! Mbali na kutumiwa katika urembo mafuta hayo yanaweza pia kutumika kupikia, kuoka au kukaanga aina mbalimbali za vyakula.

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa matumizi ya mafuta haya katika mapishi huwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuimarisha afya ya moyo.

“Lauric Acid’ iliyomo kwenye mafuta ya nazi inasaidia kudhibiti kiwango cha kolesteroli kwa kuongeza kolesteroli nzuri (HDL) na kupunguza ile mbaya (LDL). Matokeo yake ni moyo wenye afya, mzunguko mzuri wa damu na mwili wenye furaha zaidi…

… Ukiyatumia kwa kiasi, mafuta haya yanaweza kuwa mbadala mzuri wa baadhi ya mafuta yaliyosindikwa kupita kiasi,” amesema Devotha Mushumbusi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC).

Pamoja na faida hizo Mushumbusi ameongeza kuwa mafuta haya yakitumika kwa kiasi husaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula na kuchochea uchakataji wa nishati (energy breakdown), jambo linalosaidia kuupa mwili nguvu na kuongeza ufanisi wa mifumo ya mwili kufanya kazi kwa usahihi.

“Kwa mtu anayetaka kupunguza uzito, mafuta haya ni msaada mzuri kwani husaidia kupunguza hamu ya kula. Pia huchangia kuchoma kolesteroli na kusaidia mwili katika mchakato wa kupungua uzito,” ameongeza Mushumbusi.

Mafuta ya nazi yanaweza pia kutumika kuaandaa saladi au mbogamboga. Picha/ Canva

Jinsi ya kutumia mafuta ya nazi jikoni

Mafuta ya nazi yanaweza kutumika kwa njia mbalimbali jikoni. Unaweza kuyatumia kukaanga samaki, viazi, au vitafunwa kwa ladha ya kipekee ya kitropiki. 

Pia, kuongeza kijiko kimoja cha mafuta haya kwenye mboga za majani au wali huboresha harufu na ladha yake. 

Kadhalika, ukichanganya kiasi kidogo cha mafuta ya nazi kwenye keki au maandazi hupata ladha tamu na ya asili inayovutia zaidi.

Mafuta ya nazi si tu kwamba yanaboresha ladha ya mapishi yako, bali pia yanalinda afya ya moyo, kusaidia kupunguza uzito, na kuupa mwili nguvu.

Kwa hivyo, kuyatumia kwa kiasi na kwa utaratibu ni njia bora ya kufurahia ladha na afya kwa pamoja jikoni mwako.

/
No matches found for this filter
29 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
29 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
29 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV

FAHAMU IDADI YA WATANZANIA WALIOOZA MENO

FAHAMU IDADI YA WATANZANIA WALIOOZA MENO

Nukta TV

"OKTOBA 29 IMTUPA FUNZO" RAIS SAMIA

"OKTOBA 29 IMTUPA FUNZO" RAIS SAMIA

Nukta TV