Dola ya Marekani yaimarika kwa Sh10 dhidi ya Shilingi ya Tanzania Mei 18, 2026

May 18, 2026 11:41 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Dola ya Marekani leo kupitia benki hizo mbili za biashara inanunuliwa kwa Sh2,570 na kuuzwa kwa Sh2,650 ukilinganisha na Sh2,640 iliyotumika kuuza na Sh2,560 kununua Mei 11, 2026

Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeimarika kiduchu dhidi ya Shilingi ya Tanzania ndani ya kipindi cha wiki moja huku sarafu nyingine zikiendelea kuonesha hali tulivu katika soko la fedha za kigeni nchini.

Kwa mujibu wa takwimu za viwango vya kubadilisha fedha katika benki ya NMB na CRDB vinavyotumika leo Mei 18, 2026, Dola ya Marekani imeongezeka kwa Sh10 kulinganisha na kiwango kilichotumika mwanzoni mwa juma lililopita.

Kwa ongezeko hilo, Dola ya Marekani leo inanunuliwa kwa Sh2,570 na kuuzwa kwa Sh2,650 ukilinganisha na Sh2,640 iliyotumika kuuza na Sh2,560 kununua Mei 11, 2026 kupitia benki hizo mbili za biashara.

Ongezeko hilo linaweza kupaisha gharama za uagizaji wa bidhaa kutoka nje kama mafuta na bidhaa nyingine muhimu, hali inayoweza kuchochea mfumuko wa bei na kuongeza mzigo kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje ya nchi.

Hata hivyo, sarafu ya Euro imepungua katika kipindi sawa na hicho ambapo katika benki ya CRDB, kiwango cha kununua euro kimeshuka kutoka Sh2,916.81 hadi Sh2,871.23 huku kiwango cha kuuza kikishuka kutoka Sh3,216.81 hadi Sh3,171.23. 

Hali kama hiyo imeonekana pia katika benki ya NMB ambapo bei ya kununua imeshuka kutoka Sh2,918 hadi Sh2,895 na bei ya kuuza kutoka Sh3,193 hadi Sh3,169.

Kwa upande wa Pound ya Uingereza (GBP) nayo pia imeshuka ikinunuliwa  kwa Sh3,318.34 kutoka Sh3,396.26 wiki iliyopita katika benki ya CRDB. Katika benki ya NMB, kiwango cha kununua kimeshuka kutoka Sh3,346 hadi Sh3,294 na kuuza kutoka Sh3,693 hadi Sh3,639.

Sarafu za kikanda zaonyesha utulivu

Kwa upande wa sarafu za kikanda, Shilingi ya Kenya (KSH) imeendelea kuwa karibu na viwango vya wiki iliyopita, ikionyesha utulivu mkubwa huku Rand ya Afrika Kusini (ZAR) na Shilingi ya Uganda zikionyesha hali sawa na hiyo.

Mwenendo huu unaashiria kuimarika kwa Shilingi ya Tanzania dhidi ya baadhi ya sarafu kama Euro na Pound katika mwanzo wa wiki hii, licha ya dola kuendelea kuonyesha nguvu ndogo sokoni.

Kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka Ulaya na Uingereza, kushuka kwa Euro na Pound kunaweza kusaidia kupunguza gharama za uagizaji. Aidha, hali hiyo inaweza kutoa nafuu kwa wasafiri na wanaofanya malipo kwa sarafu hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

Nukta TV

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV