Viwango vya kubadilisha fedha Tanzania Aprili 22, 2026
Viwango vya kubadilisha fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania vinavyotumika leo Aprili 22, 2026 vimeendelea kuwa tulivu kwa baadhi ya sarafu bila kuonyesha mabadiliko yoyote kulinganisha na vile vilivyokuwa vikitumika jana.
Kwa mujibu wa takwimu za viwango hivyo kutoka benki za CRDB na NMB, thamani ya sarafu mbalimbali dhidi ya Shilingi ya Tanzania imebaki ile ile kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa.
Mathalani, Dola ya Marekani leo imenunuliwa kwa Sh2,570 na kuuzwa kwa Sh2,650 kupitia Benki ya CRDB na NMB ikiwa ni sawa na kiwango kile kilichorekodiwa jana na wiki iliyopita.
Hali hii inaashiria mwenendo thabiti wa soko la fedha za kigeni nchini, ingawa viwango hivi huweza kubadilika kila siku kulingana na nguvu ya mahitaji na upatikanaji wa fedha za kigeni.
Hata hivyo, kuna ongezeko kiduchu la Sh2.01 kwenye pauni ya Uingereza ambapo kwa mujibu wa Benki za CRDB na NMB jana ilikuwa ikiuzwa kwa Sh3,370.36 na kununuliwa kwa Sh3,670.36 na leo imeuzwa kwa Sh3,372.37 na kununuliwa kwa Sh3,672.37.
Kwa wafanyabiashara, wawekezaji na walipakodi, taarifa hizi ni muhimu katika kupanga shughuli za kifedha kama malipo ya ada, kodi na manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya nchi.
Aidha, sarafu nyingine kutoka mataifa kama China, Afrika Kusini na India nazo zimeendelea kudumisha viwango vilevile bila mabadiliko, huku sarafu ya nchi za Umoja wa Ulaya ikiongezeka kwa Sh0.74 kutoka kiwango kilichokuwepo jana.

Latest