Dk Nchemba aagiza Sh200 bilioni za Rais Samia kusimamiwa vizuri
- Aelekeza fedha hizo kutumika katika miradi yenye tija.
- Aonya dhidi ya mikopo inayonyonya wananchi maarufu kausha damu.
Dar es Salaam. Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amezitaka wizara, taasisi na mamlaka zote zinazohusika ksimamia vyema utolewaji wa Sh200 bilioni zilizoahidiwa na Rais Samia Suluhu kwa kundi la wanawake na vijana ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa makundi hayo.
Dk Nchemba ametoa agizo hilo leo Februari 5, 2026, jijini Dodoma, akieleza kuwa fedha hizo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia ndani ya siku 100 tangu kuanza kwa muhula wake wa pilii wa uongozi.
“Utoaji wa hundi ya Sh200 bilioni unaonyesha kwa vitendo kwamba Serikali ya awamu ya sita inatekeleza ahadinzake kwa vitendo na sio tu ahadi, na sio tu maneno…
…Tukio hili linaweka msingi mpya wa kuimarisha ushiriki wa vijana na wanawake katika uchumi wa Taifa na kuharakisha Tanzania kuelekea katika sera ya uchumi jumuishi,” ameeleza Dk Nchemba wakati wa hafla ya makabidhiano ya fedha hizo.

Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka, hundi ya Sh200 bilioni.Picha/owm.
Fedha hizo ni zile zilizoahidiwa na Rais Samia Suluhu wakati analihutubia Bunge kwa mara ya kwanza Novemba 14, 2026 ikiwa ni miongoni mwa mikakati mahsusi ya Serikali ya kuongeza ukwasi na ujumuishi wa kiuchumi kwa wanawake na vijana na walemavu.
Kabla ya Rais Samia kuahidi fedha hizo, makundi hayo yalikuwa yakitegemea uwezeshwaji kupitia mikopo ya asilimia 10 iliyokuwa ikitolewa na halmashauri zote 128 nchini kabla ya utaratibu huo kuhamishiwa katika taasisi za kifedha ikiwemo benki.
Lengo la Serikali kuhamishia utaratibu huo benki lilikuwa ni kupunguza ubadhirifu na tabia ya baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo kutokuirudisha kwa wakati suala lililowanyima fursa wahitaji wengine kunufaika.
“Rais hajataka fedha zikae Serikalini mara zote tangu ashike wadhifa wa kuongoza nchi hii amekuwa akielekeza fedha ziende kwenye miradi iliyokusudiwa yenye matokeo. Rais hajakusudia ziende kwenye vikundi hewa ,” amesisitiza Dk Nchemba.
Licha ya mikopo hiyo kuhamishiwa katika taasisi za kifedha bado baadhi ya Watanzania wamelalamikia mlolongo mrefu na masharti magumu wanayopewa wakihitaji mikopo hiyo suala linalowafanya kushindwa kuipata kwa wakati
Akiangazia suala hilo Dk Nchemba ametoa wito kwa taasisi za fedha kuweka masharti nafuu kukawezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na mikopo hiyo huku akionya dhidi ya mikopo isiyo rasmi inayotoza riba kubwa maarufu kama kausha damu.
Latest