Jenista Mhagama afariki dunia
- Taratibu za mazishi kutangazwa hivi karibuni.
Arusha. Spika wa Bunge la Tanzania Azzan Zungu ametangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea Desemba 11, 2025 Jijini Dodoma.
Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Elimu kwa Umma Ofisi ya Bunge iliyotolewa leo Desemba 12, 2025 imethibisha kifo hicho, huku Spika wa Bunge akitoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Peramiho, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.
Aidha, Ofisi ya Bunge imebainisha kuwa inaratibu mipango ya mazishi kwa kushirikiana na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zitaendelea kutolewa
Mwanzo mwisho safari ya Mhagama
Jenista ni miongoni mwa wabunge wakongwe katika historia ya Tanzania akiingia bungeni kama mbunge wa Viti Maalum mwaka 2000 na mwaka 2005 alichaguliwa kuliongoza jimbo la Permiho lililopo Songea nafasi aliyoitumikia mpaka anafikwa na umauti.
Alianza kujihusisha rasmi katika siasa mwaka 1987 kupitia umoja wa wanawake na vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM hadi kushika nyadhifa kubwa zaidi za nchi kwa tiketi ya chama hicho.
Nyota ya Mhagama ilingaa katika awamu tatu za uongozi kuanzia ile ya Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli na katika awamu ya kwanza ya Rais Samia Suluhu Hassan akihudumu nyadhifa za juu Serikalini.
Mwaka 2014 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi hadi 2015 alipoachia kijiti hicho kupisha uchaguzi mkuu na kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri.
Mwaka 2025 baada yabuchaguzi aliingia tena katika baraza la mawaziri, alipoteuliwa kuwa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu katika Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Rais John Magufuli na baadae chini ya Rais Samia mpaka Januari 10, 2022.
Kuanzia Januari 2022, Mhagama alihudumu kama Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora na baadaye kama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kuanzia Aprili 02, 2023.4
Mwaka 2024 alipelekwa Wizara ya Afya kuziba nafasi ya Ummy Mwalimu, nafasi aliyoitumikia hadi mwishoni mwa mwaka huu, Tanzania ilipofanya Uchaguzi Mkuu.
Katika awamu ya pili ya uongozi wa Rais Samia Jenista amekuwa miongoni mwa wabunge nane waliowekwa kando katika orodha mpya ya baraza la Mawaziri iiliyotolewa na kiongozi huyo wa nchi suala lilomfanya kusalia kuwa mbunge wa kawaida.
Latest