Rais Samia kuhutubia Taifa kupitia wazee wa Dar kesho Desemba 2

December 1, 2025 2:29 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni moja kati ya hatua anazochukua Rais Samia kuhakikisha nchi inarejea katika amani. 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,anatarajiwa kuhutubia Taifa kesho, Desemba 2, 2025, atakapokuwa anazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa tano asubuhi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Desemba 1, 2025 amesema hotuba ya Rais na mazungumzo hayo ni moja kati ya hatua anazochukua Rais Samia kuhakikisha nchi inarejea katika amani. 

“Ni mkutano muafaka unaorejesha matumaini na kuendelea kuponya pale ambapo Watanzania waliumia,” amesema Chalamila.

Hata hivyo, Chalamila amesema hatua ya Rais Samia kuhutubia Taifa katika jiji la Dar es salaam imechochewa na hali ya amani na utulivu inayoendelea kutengemaa jijini humo akitoa wito kwa wananchi kutumia nafasi hiyo kumsikiliza. 

Itakumbukwa kuwa, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kukutana na makundi ya kijamii tangu aapishwe kuwa Rais wa Tanzania kwa muhula wa pili, Novemba 3, 2025. 

Rais Samia anatarajiwa kuhutubia Taifa katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kuponya majeraha ya matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea kufuatia  maandamano ya Oktoba 29.

Vurugu zilizotokea zilisababisha maafa mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali binafsi na za umma pamoja watu kupoteza maisha ambapo bado Serikali haijaweka bayana idadi ya vifo.

Aidha, viongozi wa Serikali wameendelea kutoa wito kwa Watanzania kutofanya tena maandamano yanayoweza kusababisha fujo kama zilizotokea, wakati kukiwa na minong’ono ya kufanyika tena kwa maandamano Desemba 9, mwaka huu.

Waziri Mkuu wa Tanzania Dk Mwigulu Nchemba alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari siku chache zilizopita alisema pamoja na Serikali kutoa wito huo, imefungua milango kwa Watanzania wenye changamoto kuziwasilisha 

/
No matches found for this filter
22 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

Nukta TV